VAZI alilotinga Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji limezua utata kufuatia kuonesha sehemu yake ya tumboni (kitovu).
Utata huo umekuja mara baada ya picha inayomuonesha mbunge huyo akiwa amejipara na kuvalia vazi hilo ambalo linamuonesha sehemu hiyo nyeti na kutupiwa mtandaoni.
“Jamani huu ni utata sasa, inakuwaje mheshimiwa anatinga vazi kama hili? Haya mambo bora angewaachia mastaa wadogo, umri wake haufanani na mambo haya!” aliandika mdau mtandaoni