MSANII asiyeishiwa na matukio, Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’ amefunguka kwamba kuharibika kwa mwili wake hasa kwenye makalio kumetokana na kuvaa nguo za ndani aina ya ‘bikini’ ambazo zimechimba mistari.
“Kwa kweli hizi nguo za ndani hasa bikini zinatuharibu sana hasa sisi tuliojaaliwa kuwa na maumbile makubwa, nilikuwa navaa lakini kwa kweli zimenichimba sana kiasi cha kuniharibu na kupoteza mvuto wangu, sivai tena…nitaangalia ustaarabu mwingine,” alisema msanii huyo