Rais
wa Tamsia Taifa, Sheikh Jaffar Said Mneke (katikati), akiongea na
waandamanaji mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa wizara.
Barua inayoonyesha madai wa waandamanaji hao.
Baadhi ya Waislamu jijini Dar es Salaam leo wameandamana kuelekea
Wizara ya Mambo ya Ndani kutaka wenzao waliokamatwa wakati wa zoezi la
Sensa ya Watu na Makazi linaloendelea nchini kuachiwa. Katika maandamano
hayo viongozi wa Waislamu na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani
walikutana na kufikia makubaliano kuwa wote waliokamatwa wakipinga zoezi
la Sensa Zanzibar na Tanzania Bara wataachia huru. Pia waandamanaji hao
wamekubaliana kufanya maandamano mengine ya kumng'oa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba kwa kutoonesha ushirikiano nao.