UKARIBU wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platinumz' na mama yake Snura Khasim 'Sandra' umewafanya baadhi ya watu kubaki midomo wazi kwa kusema kuwa wanaishi maisha ya kizungu mno.
Hivi karibuni mwandishi alitimba nyumbani kwa staa huyo pande za Sinza Mori jijini Dar na kuwashuhudia wawili hao wakijiachia huku wakifanyiana vituko vya utani na kufikia kupigana mabusu ambayo ni nadra sana kuonekana katika familia za Kitanzania.
“Diamond na mama yake kwa kweli wanaishi maisha ya raha sana, kama hujaambiwa huwezi kudhani kama ni mtu na mama yake wanataniana sana, wanaishi kizungu,” alisema mmoja wa jirani yao kabla Ijumaa halijashudia laivu vituko hivyo.
Jirani huyo alisema kuwa maisha hayo ya Diamond na mama yake yalianza muda mrefu kabla hata nyota ya Diamond haijang’aa katika ulimwengu wa muziki.
MSIKIE DADA WA DIAMOND
Dada wa Diamond anayefahamika kwa jina la Esma, alizungumza na paparazi wetu kuhusiana na maisha ya wawili hao ambapo alisema wanaishi kizungu kwani huwezi kukuta mtu anakuwa na sheria kali kama zile za wazazi wa kizamani.
“Siyo wao peke yao, familia nzima tunaishi kirafiki sana, ukimkuta mama, mimi, mjomba, Diamond au hata madensa wa Diamond jinsi tunavyotaniana na kucheka huwezi kuamini,” alisema Esma.
PICHA MPYA
Wanndishi lilipotimba katika nyumba hiyo lilikutana na hali hiyo ambapo Diamond na mama yake walijiachia na kupigana mabusu ambayo kimsingi yanaweza kuzua maswali kwa mtu anayewashuhudia kwa mara ya kwanza.
Mwandishi wa gazeti hili hakubaki nyuma, alifotoa picha za kutosha huku wawili hao wakiwa hawana wasiwasi wowote.
MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
Akizungumza na mwandishi, mama Diamond alisema kwenye familia yao wamekuwa wakiishi kama marafiki tangu kitambo na hiyo ndiyo staili ya maisha yao hata kabla Diamond hajawa maarufu.
“Tumeishi hivi tangu siku nyingi, ukitukuta nyumbani ni kama vile marafiki kumbe mtu na mama yake. Si kwa Diamond tu hata kwa watu wetu wa karibu kama madensa wa Diamond yaani ni full burudani nyumbani,” alisema mama Diamond.