Friday, August 31, 2012

DR SLAA AJIBU MAPIGO

          Dr.Slaa akiongea na wandishi wa habari leo mjini Iringa.

Mh Samweli Sitta kwa maneno yake aliyotamka hivi karibuni kama ilivyo ripotiwa na vyombo vya Habari nchini. Dr alieleza hayoleo mbele ya waandishi wa habari mjini Iringa katika ukumbi wa M.R HOTEL Majira ya asubuhi alianza kwakukanusha uongo aliousema Mh Sitta kuwa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo hamna viongozi tishio ila ni Dr Slaa.Amemshangaa nakusema, ajuavyo yeye Hawezi kuwasemea akikanusha hayo pamoja na kumuita Mh mwenyekiti wa Chadema ni mchezesha disco katika nchi hii niuwongo ulio wazi. Tunavyojua MH Mbowe nimmiliki wa klabu ya burudani ambamo wapenzi wa mziki katika nchihii wanajua hivyo natena kunabaadhi ya Mawaziri ni wateja katika ukumbihuo.

Akimuelezea Mh Samweli Sita ni Muhaini wa kwanza katika nchi hii akiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri la muungano wa Tanzania alizuia muswada uliopelekwa Bungeni na Mh Zito kabwe unaohusu Ufisadi katika makampuni yauma. Yakiwemo Meremeta nk.kinyume chake wakamfukuza Mh zito Bungeni kwa miezi sita na wakamrudisha kimyakimya.

Pia Mh sita nimwanzilishi wa chama cha CCJ katika nchi hii wakiwa na Mh Mwakyembe  kwa  lengo lakuhama CCM waliandika katiba kama ya CHADEMA wakiwa nadhamira ya kujaribu upinzani huku wakisema wakishindwa watajiunga na CHADEMA. Wakatihuo Sitta akifanya mawasiliano ya faragha maranyingi na Dr.Slaa  huku akijigamba kuwa ana  wa bunge wengi zaidi ya Hamsini atahama nao iwapo atakuja Chadema.

 kipindi cha uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamuhuri la Muungano CCM walipo badili utaratibu na kumtaka mgombea Mwanamke yeye alichukizwa nahilo. Nandio ulikuwa mwanzo wakutapatapa akijua muda wake wakudhani yeye ni Spika wakudumu. Kwani mfano tunao akiwa spika alijenga nyumba ya Spika Jimboni kwake kwa pesa ya Serikali yenye gharama kubwa zaidi ya mara kumi yakiwango kilicho pangwa cha kujengewa ofisi za wa Bunge katika kila jimbo. Nasiyo kama alivyofanya yeye. Dr Saa alisema tunayajua mengi yafanywayo na viongozi serikalini wanao toka CCM kwaleo nasema machache mengine ni akiba. kwakua natumia silaha sawa na wanyotumia maadui zetu.

Pamoja na hayo Chadema wamewashukuru Jeshi la Polisi na CCM Kwakuwa wamekuwa kama  makada wao kwani wamewafanya wawafikie wananchi wegi katika mkoa wa Iringa baada ya kusitisha Maandamano na Mkutano mpaka Sensa ipite wao wakaamua kwenda mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji. kata kwa kata hivyo toka waanze wamefika vijiji Mia na  hamsini katika Wilaya ya Mufindi,(W)Iringa,Wilaya ya Kilolo pamoja na Iringa Manispaa ambapo watafanya Mkutano tar 9.9.2012 viwanja vya Mwembetogwa.

Picha na habari- Said Ng'amilo wa Mjengwablog, Iringa



Love to hear what you think!