KIJANA mmoja wa kiume
aliyedaiwa kuwa ni mfanyabiashara ndogondogo amekutwa amefariki katika
kituo cha mabasi yaendayo kasi Manzese, jijini Dar, leo asubuhi.
Inasemekana vijana wengi huwa wana tabia ya kulala ndani ya vituo hivyo
kwa hiyo watu iliwachukua muda mrefu kubaini kama amefariki.
Kwa mujibu wa mtendaji wa serikali wa Kata
ya Midizini-Manzese, Penford Kizo na mashuhuda wengine, kifo cha kijana
huyo hakijafahamika kimesababishwa na nini.
(Picha / Habari: Gabriel Ng’osha na Mussa Mateja / GPL)