Asubuhi ya leo kumezagaa taarifa kuwa mwanamuziki mkongwe wa Taarab wa Zanzibar, Bi. Kidude amefariki dunia. Radio ya Zenji FM ya visiwani humo nayo ilitangaza kifo chake. Lakini kutokana na vyanzo mbalimbali vya uhakika akiwemo mjukuu wake, Bi. Kidude bado yupo hai.
Mo Blog: Habari zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa mkongwe wa muziki wa jadi visiwani Zanzibar Bi. Kidude amefariki dunia si za kweli MO BLOG imezungumza na watu wa karibu ambao wamesema kwamba Bi. Kidude bado anavuta pumzi na amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo visiwani humo.