Monday, July 23, 2012

WAZIRI ZANZBAR AJIUZULU KUTOKANA NA AJALI YA MV SKAGIT


.
Ikiwa ni siku ya sita toka kuzama kwa MV SKAGIT huko Zanzibar na kusababisha vifo vya watu 78 mpaka sasa, Waziri wa Miundombinu na mawasiliano wa serikali ya mapinduzi Zanzibar HAMAD MASOUD HAMAD ambae pia ni mwakilishi wa jimbo la Ole Kaskazini Pemba, ameamua kujiuzulu.
Baada ya kujiuzulu nafasi yake imechukuliwa na RASHID SEIF SULEIMAN ambae ni mwakilishi wa jimbo la Ziwani mkoa wa kusini Pemba.
Mwandishi Khaleed kutoka Zanzibar amesema “ni kweli nimepata taarifa za kujiuzulu kwa Waziri huyo, aliandika barua ya maombi ya kujiuzulu kwa Mh Rais na barua hiyo leo ndio amejibiwa rasmi, alishajiuzulu toka saa 12 leo jioni ambapo wananchi wa Zanzibar walimuandama sana ndio kisa cha kujiuzulu”
“Wananchi walifurahi sana kwa kujiuzulu kwake kwa sababu hana umuhimu kwenye utendaji kazi wake, kila mtu kafurahi sana na mpaka sasa zinafanywa sherehe mbalimbali kwa kujiuzulu kwa waziri huyo, kulikua kuna vurugu la uamsho lakini mpaka sasa tunamshukuru Mwenyezi Mungu Zanzibar hali ni shwari hakuna vurugu ya aina yoyote wala barabara kuchomwa na kupangwa mawe” KhaleedW



Love to hear what you think!