Friday, July 20, 2012

DUDE AMDISS FLORA MVUNGI

 
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
 
Flora Mvungi.
Na Erick Evarist
ACTOR wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenyanyua kinywa chake na kumchana mwigizaji, Flora Mvungi kuwa amepotoka kimaadili.
Katika mahojiano aliyoyafanya Dude na paparazi wetu juzikati jijini Dar, alisema kuwa Flora ni kama mwanaye kwenye fani hivyo akiona anaingia katika mambo yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania, lazima ampe ukweli.
Dude alitiririka kuwa, amesikitika sana kusikia hivi karibuni Flora alijiingiza katika mabishano aliyoyaita ya kijinga na msanii mwenzake Irene Uwoya kiasi cha kufikia hatua ya kuanika siri zake za chumbani.
“Kuanza kumjibu Uwoya kwamba H Baba anajua mapenzi kwenye midia na kuanika mambo yake ya ndani ni vitu ambavyo havina maana katika jamii, kwani angenyamaza kimya angepungua nini?,” alihoji Dude.
Akaongeza kuwa, ifike mahali wasanii waangalie mambo ya kuongea mbele za watu na yapi yabaki siri yao kwani mengine kuyaanika ni sawa na kujivua nguo.




Love to hear what you think!