Tuesday, July 24, 2012

KUNDI LA MTANASHATI LATIKISA JIJINI ARUSHA‏

 
Msanii nyota wa kundi la Mtanashati la jijini Dar, PNC akifanya vitu vyake katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abed.
 
Kundi la Mtanashati likitambulishwa uwanjani hapo kabla ya kufanya vitu vyake.

 
Msanii wa Arusha Rama D naye alikuwepo, akifanya mambo uwanjani hapo.
 
Msanii Happy kutoka kundi la Mtanashati akikonga nyoyo za mashabiki wa Arusha, huku akimdatisha shabiki huyo aliyepanda jukwaani na kumtunza kiaina.
 
Msanii wa Maigizo na Muziki, Kitale akifanya vitu vyake na wimbo wake wa ''Hili dege nomaaa''.
Msanii Kitale akiruka kama Joti na kuwafanya wapenzi wa muziki wake kuchanganyikiwa.
 
PNC akilishambulia jukwaa na kuwadatisha mashabiki.
 
Msani Amazoni kushoto akishambulia jukwaa na PNC wa kundi la Mtanashati.
 
Msanii Happy akipagawisha mashabiki wa Arusha.
-----

Kundi la muziki wa kizazi kipya la jijini Dar es Salaam, Mtanashati Entertainment, juzi lilikonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo  jijini Arusha katika tamasha la uzinduzi wa 'Documentary' ya kupinga mauaji ya albino na ongezeko la watoto wa mtaani.

Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja wa mpira  wa Sheikh Amri Abed na kuandaliwa na Victoria Home Theater kwa kushirikiana na Manispaa ya jiji la Arusha.

Kundi hilo likiongozwa  na msanii PNC na wasanii wengine mahiri, lilitoa burudani ya kukata na shoka na kuwapagawisha mashabiki wake wakiwemo waheshimiwa madiwani waliohudhuria uzinduzi huo na kujikuta wakizitupa suti zao na kuanza kusakata muziki huo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kundi hilo, Ustaadh Juma Namsoma, alisema kuwa burudani iliyotolewa na kundi lake ni mwendelezo wa burudani za uhakika katika kukabiliana na ushindani wa muziki wa kizazi kipya.

Alisema kwa sasa kundi hilo kwa kutumia wasanii wake, PNC, Amazon, Suma Mnazaleti, Yfil Davi na mwanadada Happy wamejipanga kutoa burudani ya kukata na shoka maeneo mbalimbali hapa nchini na kwamba wapenzi wa kundi hilo wajiandae kupata burudani ya uhakika.

Alisema kwa sasa kundi hilo linatamba na nyimbo zake mpya kupitia wasanii hao na wanajiandaa kuzitambulisha muda mfupi baada ya kuipua jikoni.
(Picha/Habari na: Joseph Ngilisho, GPL / Arusha)



Love to hear what you think!