Friday, July 27, 2012

JB ATOA WOSIA

 
Jacob Steven ‘JB’.
Na George Kayala
MKONGWE wa sanaa ya maigizo nchini, Jacob Steven ‘JB’ ametoa wosia kwa rafiki zake ambao watatakiwa kuufuata siku atakapolala katika nyumba yake ya milele.
Akizungumza na Mwandishi hivi karibuni jijini Dar, JB alisema neno la mwisho ambalo atapenda rafiki zake walizingatie ni kushikamana na Mungu aliye hai na kuwa na toba kila iitwapo leo.
“Hakuna ajuaye siku ya kufa kwake. Wakati wowote nikiondoka duniani nitapenda rafiki zangu wote washikamane na Mungu na kuwa na toba ya kweli kila kukicha ili nao siku moja waje kuurithi uzima wa milele,” alisema JB.
Pamoja na wosia huo kwa rafiki zake, JB amewataka wasanii wenzake kuwa wacha Mungu siku zote ili pale umauti utakapowakuta wawe na tumaini la kuwa na maisha mazuri baada ya kif


Love to hear what you think!