Monday, September 30, 2013

TAARIFA INAYOSEMA HUENDA MAGAIDI WA WESTGATE WALITOROKEA NJIA YA MAJI TAKA CHINI YA JENGO HII HAPA

Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.

Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.

Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.


Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.

Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.


Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.

Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi

-BONGO5Love to hear what you think!