Saturday, April 20, 2013

Kwanini Serukamba Hakutolewa Bungeni?

Nyerere: "waswahili wana mambo ya ajabu. mambo ya kijinga jinga yakisemwa kwa kiingereza, wanashangilia kana kwamba ni mambo mema"

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema baba wa taifa Mwl Julius K. Nyerere katika moja ya hotuba zake.
Tusi alilolitoa Serukamba ndio tusi kubwa kuliko yote yaliyowahi kutolewa bungeni mpaka sasa. Tofauti na mengine yeye lake amelitoa kwa kiingereza kiasi kwamba naibu spika ameliona ni jema hivyo kutomchukulia hatua yoyote.

Hata majadiliano yanayoendelea sasa miongoni mwa wananchi na viongozi ni kuhusu "utovu wa nidhamu" wa Tundu Lissu wa kuomba miongozo na taarifa kila mara hivyo kutimuliwa bungeni na wenzake waliokuwa wakipinga kitendo cha naibu spika kumtoa nje. Hili la Serukamba halizungumzwi kama ni tusi kuu bungeni.

Tatizo ni kama alivyosema Nyerere, katukana kwa kiingereza hivyo spika na naibu wake hawaoni kuwa ni tusi. Waziri mkuu haoni kuwa ni tusi. Aibu!


Love to hear what you think!