Wednesday, April 17, 2013

JOKATE ANASWA KIMAHABA NA MWANAUME

PICHA ya Miss Temeke 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti‘ akiwa na mwanaume kimahaba imenaswa na kufi kishwa kwenye dawati la Waandishi.

Chanzo makini kimeitonya Centre Spread kuwa Jokate ameamua kujiweka kwa mwanaume huyo ambaye hakufahamika ili kulipa kisasi kwa aliyekuwa mpenzi wake,

Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alimuacha na kumchukua Peniel Mungilwa ‘Penny’.
Baada ya kuinasa picha hiyo kwenye vyanzo vyake, paparazi wetu alimuendea hewani Jokate na kumshushia tuhuma hizo ambapo alileta hadithi njoo, utamu kolea:
“Unajua kwa sasa nimeingia kwenye muziki na hivi karibuni nitatoa video yangu, unajua lazima kubadili fani, ndiyo maisha ya siku hizi na huyo mtu nimefanya naye video,” alisema Jokate kisha akakata simu.


Love to hear what you think!