MSANII wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto
yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru
Mungu, Risasi Jumamosi lina data kamili.
Matukio hayo
yaliyoshuhudiwa na wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo
Shilole alikuwa akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.
MCHANAMajira
ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake
Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha
akapata…
Stori:Gladness Malya na Hamida HassanMSANII
wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima
mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu,
Risasi Jumamosi lina data kamili.
Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na
wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa
akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.
MCHANAMajira
ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake
Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha
akapata nao msosi na kuwapa msaada wa vyakula.
Wakati wa mchana,
Shilole alionekana akiwa ndani ya mavazi nadhifu yaliyomsitiri vilivyo
binti wa Kiislamu, akila pamoja na watoto hao na wageni wengine waalikwa
wakiwemo wasanii wenzake.
USIKUKweli
usiku ni wa mashetani kwani baada ya matukio ya mchana, sherehe
ilihamia katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo kulikuwa na
matukio kibao ya kumkufuru Mungu.
SHEREHE YAANZASherehe
hiyo ilianza majira ya saa 4:00 usiku kwa wageni waalikwa kuanza
kupombeka kwa ‘mipombe’ mikali kwani hakukuwa na zile za kawaida huku
wakipata muziki mtamu wa kushushia ulabu tumboni.
JUU YA MEZA Kufuatia kukolea kwa kinywaji, Shilole alipanda juu ya meza na kuanza kukata mauno kihasarahasara.
MASHINDANO YA KUKATIKABaadhi
ya waalikwa ambao nao walikuwa wamekolea masanga tilalila, walianza
kushindana kukata mauno huku mshehereshaji wa shughuli hiyo, Halima
Haroun ‘Kimwana Manywele’ akimnyanyua mtu mmojammoja kwenye kiti na
kwenda kukata mauno mbele na ambaye alishindwa, basi alitakiwa atoe Sh.
elfu 50.
Katika kukata mauno, kuna baadhi ya waalikwa waliopitiliza
na kujikuta wakimwaga ‘lazi’ na kucheza kwa staili ya kubinuka wakiwemo
kuku watamu (mashoga) na mastaa wa filamu kama Jacqueline Wolper, Halima
Yahaya ‘Davina’, Batuli ‘Neshi’, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’, Baby
Candy na wengine kibao.
Pamoja na kufuru hizo pia kulikuwa na matukio
mbalimbali kama ugomvi baada ya Shilole kupoteza simu na kuanza
kumshushia kipigo mdogo wake anayejulikana kwa jina moja la Mary.
Pia
mwanadada anayewatengeneza wasanii nywele anayejulikana kwa jina moja
la Bonita, alidai kumfumania mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la
Papaa akiwa chobingo na ‘mchuchu’ mwingine hivyo pakachimbika.
Hata hivyo, waliokuwa wakimwaga ‘lazi’ ni walewale waliokuwa kwenye kisomo mchana na kuonekana kusahau mambo ya dua.