Tuesday, July 31, 2012

UTAPELI WA CHAMELEONE KWA SHIGONGO



Joseph Mayanja Chameleone.

Jean Pierre Nimbona ‘Kidum’.
MWANAMUZIKI Mganda mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone, amezidi kutupambanua Watanzania. Sakata lake la kuiibia Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, limedhihirisha kuwa wana wa taifa lililokombolewa na Mwalimu Julius Nyerere ‘JK’, hatupo wamoja.
Limetoa tafsiri kwamba Watanzania wengi ni makini lakini tatizo kuna wachache ambao huamua kupotosha wengi kwa kueneza uzushi. Hao ni wale wapekepeke au viherehere, wanaojifanya wana utandawazi kwa kueneza uzushi mitandaoni.
Kundi hilo dogo la wapekepeke au mashakunaku katika muonekano wa kileo (wakijifanya wajuzi wa kutumia mitandao ya intaneti), waliwapotosha Watanzania wengi kuhusu mwanamuziki huyo tapeli, mkorofi, mwenye tamaa, mdokozi, mtukutu na maneno mengine chanya na hayo.
Wakazusha kwamba eti, Chameleone amenyang’anywa hati ya kusafiria na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo. Yaani mtu mwenye hulka ya utapeli amezusha uongo kama ilivyo asili yake, halafu watu wachache wanashupalia kuueneza ili kupotosha ukweli.
Naomba niweke kweupe kwamba Chameleone ni tapeli. Ametenda uovu mkubwa kwa Watanzania, vilevile amemfedhehesha hata mwanamuziki mwenzake, Jean Pierre Nimbona ‘Kidum’, kwani yeye ndiye aliyesimamia malipo yote kuhakikisha kwamba Chameleone anakuja nchini kufanya shoo Julai 7, mwaka huu.
Labda nitambulishe kwamba shoo inayozungumzwa hapa ni lile Tamasha la Usiku wa Matumaini, lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Chameleone alikuja lakini Watanzania wengi hawatambui siri nyuma ya mwanamuziki huyo kuja nchini. Hawajui kama alishatapeli, alishaitesa na kuipa usumbufu mkubwa Global Publishers.
Wasifu wa Global Publishers katika kuihudumia jamii ya Watanzania kwa takriban miaka 15 sasa, ingetosha kuwafanya Watanzania wajiulize, kweli ni Shigongo huyuhuyu leo amegeuka mbabe, kiasi cha kumnyanyasa mwanamuziki ambaye amefanya naye kazi.
Ni suala la kujiuliza, Shigongo huyu ambaye amekuwa akiendesha harakati mbalimbali za kuwakomboa vijana, wajane, yatima na watu wa kada nyingine mbalimbali, anawezaje leo kugeuka ghafla na kuwa mkandamizaji kwa watu wengine? Swali hilo tu lilitosha kutilia shaka maneno ya Chameleone.
Ajabu ni kuwa Watanzania wanamjua mtu wao ambaye wameishi naye lakini kikundi cha wapekepeke wachache, wenye hulka ya kukenua pale wanapowaona wenzao wakiharibikiwa, ndiyo haohao wakataka kuwaambukiza ujinga Watanzania ili waamini uzushi wa Chameleone.
Mimi siamini lakini wakati mwingine huwa inaingia akilini kuwa ule msemo wa “aliye juu mngoje chini” ndiyo unaotuharibu. Kwamba mtu anayefanikiwa, usihangaike kusaka na wewe mafanikio yako, badala yake, mngoje tu chini ili muogelee pamoja kweye lindi la umaskini.
Msemo huo ndiyo umewapumbaza wengi kutoweka jitihada za kufanikiwa, badala yake wale wanaofanikiwa, watafitiniwa kwa majungu, wataombewa mabaya, watapigwa misumari ili mwisho nao waanguke. Mwisho msemo aliye juu mngoje chini utimie.
Hatutakiwi kuwa hivyo, Watanzania wanapaswa kuwa wamoja katika masuala mbalimbali. Hivi sasa, pamoja na ukweli kwamba Waganda wanamjua Chameleone alivyo tapeli, msumbufu kwa mapromota lakini bado wanamuunga mkono kwenye sakata hili.
Shigongo ambaye hajawahi kuwa na rekodi ya kuwanyanyasa wageni, kuwadhulumu malipo yao au kuwafanyia jambo lolote linalofanana na hilo, leo Watanzania wenzake wanamgeuka. Wachache wasio na uungwana wanaamua kutukana kabisa. Inashangaza kupita kiasi.
CHAMELEONE ALIFANYA UTAPELI UPI HASA? KIDUMU ALIHUSIKAJE?
Alichofanya Chameleone kinajulikana lakini kabla ya kueleza kinagaubaga, naomba nimnukuu DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, ambaye naye aliweka wazi utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na Chameleone.
Ijumaa iliyopita, JD, aliwaeleza waandishi wa habari, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005.
Alisema: “Niliwasiliana na Chameleone moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana tena na hata simu yangu akawa hapokei.
“Aliendelea kunikimbia hivyo. Tatizo kubwa lipo kwa mapromota wa Kitanzania, hatuna ushirikiano kabisa. Kila alipokuja nchini kufanya shoo, nilimfuata promota husika lakini promota mwenyewe alimficha Chameleone asikamatwe.
“Mwaka 2006, Chameleone alikuja nchini kwenye shoo fulani. Kama kawaida yake alijitahidi sana kujificha nisimfikie. Hata hivyo, pamoja na kujificha kwake, nilipewa taarifa usiku kwamba yupo Bilicanas. Nikawataarifu polisi tukaenda kumkamata.
“Chameleone aliponiona alinikimbia. Ndugu zangu, Chameleone alikimbia kama mwizi. Pale Bilicanas walikuwepo Rita Paulsen wa BSS na Merey Balhabou. Wakati polisi wamemkamata, Chameleone alikubali namdai dola 3,000 na akakubali kulipa.
“Kusikia hivyo, Rita na Merey wakaniomba nimsamehe kwa sababu mtu mwenyewe amekubali kulipa. Nikawaambia ameshanisumbua sana, Merey akasema kama hatalipa, basi yeye atamlipia. Akanisihi sana kuwa mimi ni mtu wa Morogoro mwenzake, kwa hiyo nimuache Chameleone.
“Nilikubali walichokisema lakini kuanzia hapo, Chameleone na Merey hawakupatikana. Merey alikuwa ‘bize’ na mambo yake, wakati Chameleone hakutaka kupokea simu yangu kabisa.
“Siku moja nilibadilisha namba ya simu nikampigia Chameleone, akapokea vizuri. Nikamkumbusha kuhusu fedha zangu, akaniambia hana uwezo wa kulipa ila anachoweza kufanya ni mimi kuandaa shoo nyingine halafu yeye atakuja ku-perform.
“Pamoja na kuahidi, kila nilipoandaa shoo, ukifika muda wake wa kuja hakufanya hivyo. Hii inamaanisha kuwa Chameleone ana tabia ya utapeli na Watanzania tunapaswa kuwa wamoja kwenye hili tatizo.”
JD alibainisha kuwa ameamua kutokeza na kueleza haya kipindi hiki ili kila mtu atambue kwamba Chameleone siyo mtu mzuri kwenye fedha na anaweza kumkana promota wakati wowote.
ITAENDELEA

Tucta kupinga sharia ya pensheni kwa maandamano


Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholus Mgaya
Zaina Malongo
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limeandaa maandamano ya amani kupinga mabadiliko ya  kupitishwa kwa sheria ya marekebisho ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Maandamano hayo yatafanyika Agosti 4 kuanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi katika Ofisi za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholus Mgaya alisema sheria ya mpya ya mifuko ya jamii inaeleza kuwa mfanyakazi mwanachama atakapotokea kuwa ameacha au ameachishwa kazi hawezi kuchukua mafao yake hadi atakapofikisha umri wa kustaafu ambao ni miaka 55 kwa hiari au miaka 60. Alisema kuwa mfanyakazi mwanachama wa mfuko wowote wa hifadhi ya jamii, akiacha au akiachishwa kazi akiwa na miaka 35 inabidi asubiri kwa miaka 20 alipwe mafao yake ya uzeeni. “Hiki ndio kipelngele cha sheria ambacho kimeleta taharuki kubwa miongoni mwa wafanyakazi wanachma wa mfuko hiyo,” alisema Mgaya.

Alisema wanatambua ukweli kuwa malipo ya uzeeni kwa mujibu wa dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya kumsaidia mwanachama aliyefikia umri wa uzeeni, hata hivyo walishabaini kuwa dhana hiyo ni vigumu kutekelezeka katika nchi yenye uchumi duni kama Tanzania.
Alisema sababu zinazosababisha ugumu huo ni kutokuwa na uhakika wa ajira, ajira kubwa hapa nchini kuwa mikononi mwa sekta binafsi, na pia mfumo wa hifadhi ya jamii kutokuwa na fao la watu wasiokuwa na ajira.

 Mgaya alisema kutokana na viwazo hivyo, hakuna utaratibu wa hifadhi kwa mwanachama aliyekosa ajira au anayetafuta katika kipindi ambacho ameachishwa kazi na kuhoji kwamba ataishije hadi kufikia miaka 55 kabla ya kupata ajira mahali pengine.

Alisema maisha ya watu hivi sasa yamezungukwa na mazingira hatarishi yenye magonjwa yasiyotibika, ajali nyingi, majanga ya moto mafuriko mambo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa umri wa kuishi.

Hata hivyo alisema wanataka kuona mabadiliko ya haraka yafanyike kwenye sheria hiyo ya hifadhi ya jamii ili fao la kujitoa liweze kurejeshwa au uandaliwe utaratibu muafaka utakaohakikisha mwanachama anarejeshewa michango yake na ya mwajiri pamoja na riba mara tu anapokoma uanachama wa mifuko hiyo.

Alisema Tucta haitasita kuchukua hatua za kisheria endapo mamlaka itaendelea kushikilia msimamo wake wa kubakiza kifungu hicho kinachomtaka mwanachama wa mfuko afikishe miaka 55 ndio alipwe mafao yake.

Aidha alisema Tucta wamesikitishwa na kushangazwa na kuwahi kutangazwa kwa mabadiliko ya sheria hiyo ya hifadhi ya jamii huku mchakato wake ukiwa bado haujakamilika baada ya kuridhiwa na Rais kama kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutangaza kwenye gazeti la Serikali.

Mgaya alisema Tucta inataka mamlaka ya mdhibiti na msimamizi wa mfuko wa hifadhi ya jamii kuchukua jukumu la kutoa elimu kwa wanachama kuhusu sheria hiyo mpya kusaidia kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima.

 Kwa upande wa Tucta Mkoa wa Dar es Salaam, Mratibu Musa Mwakalinga alisema wanapinga mabadiliko hayo kwani mishahara ya wafanyakazi walio wengi haiwatoshelezi hivyo watakosa mtaji wa kuanzisha ujasiriamali au kujiajiri wenyewe na kujikwamua baada ya ajira kukoma. Alisema mabadiliko hayo yataongeza umasikini kwa wafanyakazi pindi watakapoachishwa au kuacha kazi, wafanyakzi wengine watakaotaka wajiajiri wenyewe pindi ajira yao itakapositishwa.
 Alisema sheria hiyo inakusudia kutotoa huduma bora zitakazokidhi mahitaji mbalimbali ya msingi wa wafanyakazi ambao ni wanachama wa mifuko hiyo inayojali zaidi wafanyabiashara, ambao sio wenye mifuko kwa kuwajengea vitega uchumi ambavyo havimnufaishi mwanachama moja kwa moja.   MWISHO

Zitto ahojiwa


Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe
Waandishi Wetu, Dar na Dodoma
SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

“Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.

Lissu ataja wengine
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha.
“Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea:

“Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”
Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50.
“Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea;

"....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”

“Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”

Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.
Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi.

“Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema.

Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”
“Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”

Majibu ya tuhuma
Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi.

“Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema).”

Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo.

"Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema

Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

Mjadala Bungeni
Mjadala huo wa wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria.

"Mheshimiwa Naibu Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?” alihoji Nassari na kuendelea:

“Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia kamati zenye mikataba.”

Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... “Tumeambiwa Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe.”

“Mimi naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,’ alisema Kessy.

Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo na baadaye apelekewe taarifa.
“Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi,” alisema.

Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui.

Alisema Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba ikibainika Bunge litawaanika hadharani.

“Kamati imerejea kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,’’ alisema Ndugai.
Naibu Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo.

Aliwatahadharisha wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya wabunge.

MAGAZETI YA LEO JULY 31

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Monday, July 30, 2012

MWALIMU APEWA KICHAPO NA WANAFUNZI KISA KAFUNDISHA WAKATI WA MGOMO

Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake

MWALIMU  mmoja  wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja  la Kahimba  wa shule ya msingi  ya Kambarage  iliyopo    Kata ya Msamala katika Halmashauri ya  Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma  amajeruhiwa vibaya  kwa kupigwa  sehemu mbalimbali za mwili  na kundi  linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao  wanadaiwa kuwa na hasira  baada  ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana  eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu  (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea  mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Kambarage  Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa  ni udhalilishaji  mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa  yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika  kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma  kutokana na Serikali  kushindwa kutimiza  ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa  inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye  eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu  mbalimbali za mwili na baadaye  alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu  wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa  mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa  wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule  za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo  wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani  ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.

Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa  ni Shule  za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana  songea.

Kwa upande wake mmoja  wa wanafunzi  wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu  wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa  wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa  ikizingatiwa kuwa  wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.

Tamimu alisema kuwa  ni vyema serikali ikatambua umuhimu  wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara  sawa na taaluma  zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.

Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea  Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu  amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule  72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo  idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu  wa shule za msingi na waratibu Elimu  kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki  kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye  Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma  Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo  huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha  80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba  ya wanachama tayari imetekeleza  kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu  CMA No: 1.

Chanzo : Wavuti

ZITTO AAHIDI KUONGEA WAANDISHI WA HABARI KESHO

 
"Kwa masaa matatu nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa zidi yangu niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu mkuu" zitto kabwe hii iko kwenye ukurasa wake wa tittwer pia ameaahidi kuwa atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho saa tano asubuhi
FUNGUA APA KUSOMA ALICHOANDIKA

RAIS KIKWETE AMZIKA SHEMEJI YAKE


Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012
 
Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea Marehemu mjini Lindi leo Julai 30, 2012.
.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Julai 30, 2012 amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.
(PICHA NA IKULU

GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA NA SERIKALI

 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
 
Uamuzi wa Serikali
Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.
Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.
Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.
Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu. 
Imetolewa na 
OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
30 Julai, 2012


ZITO ZUBERI KABWE..ATOA ONYO KALI HILI HAPA


UJUMBE WA ZITTO KWA MASWI(KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI)

"Maswi,sijawahi kugombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana.Tuhuma ambazo wewe na waziri wako mnatoa dhidi yangu uongo,uzushi na za kupikwa.Mwambie waziri wako na wewe binafsi,sijawahi kushindwa vita dhidi ya kulinda credibility yangu.Sipendi ujinga hata kidogo.Mimi sina bei.Tupambane tu tuone nani ataumia"
UJUMBE WA ZITTO KWA MASWI(KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI)
"Maswi,sijawahi kugombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana.Tuhuma ambazo wewe na waziri wako mnatoa dhidi yangu uongo,uzushi na za kupikwa.Mwambie waziri wako na wewe binafsi,sijawahi kushindwa vita dhidi ya kulinda credibility yangu.Sipendi ujinga hata kidogo.Mimi sina bei.Tupambane tu tuone nani ataumia"

YANGA YAPEWA KOMBE FAKE


Kocha wa Yanga Tom Saintfiet, akiwa na Kombe la Kagame wakati wakishangilia ushindi huo.
Na John Joseph
YANGA imetwaa ubingwa wa Kombe la Kagame 2012 juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar lakini habari ya kushangaza ni kuwa klabu hiyo imekabidhiwa kombe lenye majina ya mabingwa wa miaka iliyopita.
Katika kombe hilo, upande mmoja ulikuwa umeandikwa mabingwa wa mwaka 2006 ambao ni Polisi ya Uganda, upande mwingine limeandikwa jina la Atraco FC ya Rwanda ambao ni mabingwa wa mwaka 2009, pia upande mwingine ukiwa na heshima ya mfadhili wa michuano hiyo, Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Aidha, upande wa mwisho katika pembe nne za kombe hilo, limeandikwa jina la Yanga kuwa ni mabingwa wa mwaka 2011, kitu ambacho kinaonyesha hakukuwa na kombe jipya au pengine walilokabidhiwa halikuwa halisi.
Wakati huohuo, maandishi ya kwenye kombe hilo ya Atraco FC, Polisi na Rais Paul Kagame yote yameandikwa kwa kifaa maalum wakati upande ambao limeandikwa jina la Yanga kuwa ni mabingwa wa mwaka 2011, imebandikwa karatasi ambayo imebanduka upande mmoja na upande mwingine umechanika.
Hali hiyo inaonyesha waandaaji wa michuano hiyo, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambao rais wao ni Leodegar Tenga hawakuwa makini kufanya kazi yao, pia ubabaishaji ulichukua nafasi yake kwa kiasi kikubwa.

ISHU YA MAFISADI:DK SLAA AONYA HAKUNA HURUMA, MSEKWA ASEMA RUSHWA ADUI WA HAKI, MBATIA ATOA WIKI MOJA SPIKA AWATAJE WOTE

Mkutano ukiendelea Bungeni




Kizitto Noya, Dodoma na Leon Bahati, Dar
VYAMA vya CCM na Chadema vimetoa onyo kali kwa wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuhongwa na baadhi ya kampuni za mafuta na kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikisema havitasita kuwawajibisha pindi tuhuma hizo zitakapothibitika.Kauli ya vyama hivyo imekuja siku moja baada ya wabunge watano, watatu wa CCM na wawili wa upinzani kudaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa, ambavyo vimesababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili majina ya wahusika yawekwe hadharani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa vyama hivyo walisema wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka bungeni.
CCM: Rushwa adui wa haki
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema chama hicho kimewaapiza wanachama wake wote kutotoa wala kupokea rushwa.
Alisema rushwa ni kosa la jinai hivyo anaamini vyombo husika vya dola vitachukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikazia kauli hiyo akisema rushwa inaelezwa katika katiba ya chama hicho kwamba ni, ‘adui wa haki’ na wanachama wote waliapishwa kuwa hawatapokea wala kutoa rushwa.
Alisema yeyote anayekwenda kinyume na kanuni za CCM, anajiweka katika kundi la wasaliti wa chama.
Alisema wabunge ni kundi maalumu nchini ambalo linalipwa vizuri ili lisimamie vyema misingi ya maendeleo ya nchi pasipo tamaa wala vishawishi hivyo wanapotajwa miongoni mwa kundi la wala rushwa, CCM kinalaani vikali tukio hilo.
Kuhusu tuhuma hizo kutajwa kuwahusisha wabunge watatu wa chama hicho, Nape aligoma akisema habari hizo siyo rasmi, hivyo hawezi kuzizungumzia.
Hata hivyo, alisema CCM kinasubiri uchunguzi ufanyike ambao  ndiyo utakaoweka bayana wahusika wa tuhuma... “Tusubiri uchunguzi ukamilike.  Idadi inawezekana ikawa hiyo au ikapungua au kuongezeka.”

Dk Slaa: Hatufumbii macho ufisadi
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Nalaani kitendo cha wabunge kuhusishwa na ufisadi hasa ikizingatiwa kwamba Chadema tumekuwa tukiupinga vikali. Tumekuwa tukipinga rushwa kwa sababu ndiyo inayoielekeza nchi pabaya… Chadema hatufumbii macho rushwa.”
Alisema tangu kuanza Bunge la 10, Chadema kimekuwa kikiona baadhi ya mambo yanayoendelea katika mhimili huo muhimu wa dola yamejaa walakini... “Ndiyo maana sisi Chadema tumekuwa tukisema Bunge limepoteza mwelekeo.”
Alisema akiwa mtendaji mkuu wa chama, anasubiri taarifa kamili kutoka katika kikao cha wabunge wa chama hicho ili kuweka wazi majina ya wahusika na kisha kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ambacho kitakaa na kuchukua hatua kali.
“Tunahitaji tupate maelezo ya kina... chama chetu hakikurupuki… Nasubiri taarifa ya kokasi ya chama. Katiba ya Chadema inatambua uwapo wa kikao cha wabunge wetu na kwa bahati nzuri, kiongozi wake mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema (Freeman Mbowe) na katibu (David) Silinde ni mbunge wetu. Tunasubiri taarifa yao.”
Alisema Chadema kina kanuni ya kudhibiti rushwa hivyo, mbunge wake akitajwa miongoni mwa wanaohusishwa na rushwa, atawajibishwa kupitia kikao cha CC ya chama hicho.
NCCR-Mageuzi  yakoleza moto

Katika hatua nyingine, Chama cha NCCR- Mageuzi jana kilikoleza moto baada ya kumtaka Spika Anne Makinda awataje wabunge hao bungeni ili wafukuzwe na kufungwa kama Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inavyotaka.
Chama hicho kimetoa wiki moja kwa Spika Makinda kufanya hivyo, kikionya kuwa vinginevyo, chenyewe kitawasilisha hoja mahususi kutaka Bunge lichukue hatua hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alitoa tamko hilo mjini Dodoma, akisema  Sheria Namba 3 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, inataka wabunge wanaothibitika kujihusisha na rushwa wafukuzwe na kufungiwa kwa kipindi cha miaka mitano.
“Ni aibu kwa Bunge, taasisi inayoitwa tukufu kuwa na mafisadi. Kitendo cha Spika kukubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na kuahidi kuzivunja nyingine, maana yake anakubali kuna mafisadi. Sisi tunamtaka atutajie wabunge hao bungeni ndani ya juma moja,” alisema Mbatia.
Mbatia aliyeongozana kwenye mkutano huo na wabunge Moses Machali wa Kasulu Mjini na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini), alisema pamoja na Bunge kuendeshwa kwa kanuni zake, kwa Tanzania kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola inaweza pia kuiga yaliyofanywa katika nchi nyingine za jumuiya hiyo, zikiwamo India na  Uingereza.
Kwa mujibu wa Sheria zinazotumika katika nchi hizo, mbunge yeyote anayethibitika kutumwa na mtu nje ya Bunge, kuongea au kuandika bungeni kwa masilahi ya mtu huyo, anapaswa kufukuzwa ubunge na kufungwa.
“Kati ya mwaka 1924 na 1956, Uingereza ilifukuza wabunge 59 na kati ya mwaka 2005 hadi sasa, Bunge la India liliwafukuza wabunge 11 baada ya kuthibitika walihongwa na wafanyabiashara kuuliza maswali binafsi,” alisema.
Mbatia aliendelea kueleza kuwa katika Bunge la Nane nchini, wabunge wanne walikamatwa na kushtakiwa, kisha chama chao CUF, kiliwazuia kujihusisha tena na siasa baada ya kubainika kuwa walifunga ndoa batili na Wasomali ili wapate hati ya kuishi nchini.
“Sasa suala hili, wabunge wote wanaohisi wamo kwenye orodha hii ya ufisadi waachie ngazi. Mbunge yeyote na wa chama chochote anayeona ameshiriki uchafu huu, kwa utashi wake aachie ngazi,” alisema na kuongeza:
“Kwa vile vyama viadilifu, waige mfano wa CUF. Bunge lichukue nafasi yake kabla hatujafunga Bunge Agosti 18 tuwe tumefanya uamuzi wa kuwafukuza.”
Mbatia alisema ili Bunge lilirudi kwenye heshima yake, Spika Makinda pia anapaswa kuzitaja kamati nyingine alizosema zinachunguzwa na ikiwezekana nazo zivunjwe ili haki itendeke.
“Sisi (NCCR-Mageuzi) tunataka pia Spika azitaje kamati hizo, ziko sita na tuseme pia kwamba hatuna imani na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Tunataka nayo ijisafishe kwanza kwa kuwa nako kuna watuhumiwa.”
“Katika hili niombe kiti cha Spika kitende haki, hata kama kuna mbunge wa NCCR-Mageuzi anahisi alishiriki ufisadi huu, awahi mapema kuondoka, hii isiwe kwa vyama vingine tu,” alisema.
Mbatia alisema suala la Tanesco ni tone tu, akisema ufisadi kwa wabunge ulianza siku nyingi na kuongeza... “Mheshimiwa Kafulila (David) aliwataja wajumbe wa Kamati ya LAAC lakini, mpaka leo hakuna kinachoendelea.”
Alisema tatizo la ufisadi kuhusisha wabunge lilianza Juni 23, 2006 siku ambayo nchi iliingia mkataba na Kampuni ya Richmond... “Kuanzia hapo kumeendelea kuwa na sintofahamu katika Wizara ya Nishati na Madini. Dawa yake ni kuweka mikakati ya Bunge kujitakasa.”

Sakata lenyewe

Wabunge hao watano (majina tunayahifadhi kwa sasa) wanatuhumiwa kutumia nafasi zao za uwakilishi bungeni au ujumbe ndani ya kamati husika, kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi wanaolihujumu shirika hilo kutoka ndani na nje.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni walisema wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini wasingependa kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka.
Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa na Mbunge wa Namtumbo (CCM),
Vita Kawawa  ambaye aliomba Spika avunje Kamati ya Nishati na kutaka pia Bunge lijadili kashfa hiyo.
“Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa Kifungu cha 55 (3) f, Mbunge au Waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe.
Sasa mimi naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo.”Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono na idadi kubwa ya wabunge , ndipo Spika Makinda aliposimama na kukubali hoja hiyo ya Mbunge Vita Kawawa na kutangaza kuivunja kamati hiyo.
Spika Makinda alisema tayari pia, ameagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi.
“Nasema kwa dhati kabisa kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge. Wabunge mkae vizuri, kama kuna baadhi yetu wanakwenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi mnawezaje kuisimamia Serikali?”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Seleman Zedi alisema ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anasubiri uamuzi wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Akihitimisha hoja ya wizara yake bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema baadhi ya wabunge ambao wanashiriki kwenye vikao vya uamuzi vya Tanesco kama wajumbe wamekuwa wakilihujumu shirika hilo kwa njia mbalimbali ikiwamo kufanya nalo biashara.
“Shirika liliwahi kulipa Paundi 50,000 za Uingereza kwa ajili ya ununuzi wa vipuri, lakini kilicholetwa nchini ni masanduku ya misumari. Nguzo hizo za umeme kuna biashara inaendelea. Tunajua kwamba nguzo hizo zinazalishwa Iringa na kupelekwa Mombasa kisha kurudishwa nchini kwa maelezo kwamba zimetoka Afrika Kusini,” alisema Profesa Muhongo.

MAGAZETI YA LEO,JULY 30

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.