Tuesday, December 25, 2012

TAMASHA LA TUSKER CARNIVAL MBEYA LAHUDURIWA NA WATU WASIOZIDI 20

BANZA STONE AKIONYESHA UMAHILI WAKE WA KUCHEZA KATIKA TAMASHA LA TUSKER LILILOFANYIKA JUMAMOSI KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU WA SOKOINE JIJINI MBEYA TAMASHA HILO LILIHUDHURIWA NA WATU WASIOZIDI ISHIRINI NI KUTOKANA NA UKATA UNAOWAKABILI  BAADHI YA WAKAZI WA MBEYA  KWAKIPINDI HIKI KINACHOKARIBIA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA X MASS
HAWA NI BAADHI YA MSHABIKI WALIOHUDHURIA TAMASHA HILO

ALLY CHOKI AKIWA NA VIJANA WAKE AKITUMBUIZA BAADHI YA WATU WALIOFIKA KATIKA TAMASHA HILO
MAPACHA WATATU WAKITUMBUIZA UWANJANI HAPO
HALI HALISI INAONEKANA UWAJANI HAPO
BAADHI YA WAPENZI WA EXTRA BONGO WAKIONGEA NA ALLY CHOKI UWANJANI HAPO

Picha na Mbeya yetu

Monday, December 24, 2012

MUME AMFUMA MKEWE AKIJIUZA

Issa Mnally na Richard Bukos
AIBU! Aibu! Aibu kuu! Mwanaume mmoja mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, aliyejulikana kwa jina moja la Ombeni amemfuma laivu mkewe aitwaye Dina, akijiuza huku akidai kuwa mama watoto wake huyo kaacha kichanga nyumbani.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri katika Barabara ya Shekilango, maeneo ya Sinza, Dar usiku mnene wa saa 8:25 kuamkia Jumamosi iliyopita.
Ombeni alidai kuwa alifika nyumbani kwake Vijana-Kinondoni, majira ya saa 6:15 usiku akitokea safarini mikoani alikoenda kikazi takribani wiki mbili zilizopita ambapo alipoingia ndani aliwakuta wanaye wamelala bila mama yao.
“Nilimwamsha ‘hausigeli’, nikamuuliza mama yupo wapi? Ndiyo akanieleza kila kitu baada ya kumtishia kumfukuza kazi. Aliniambia siku hizi mke wangu anajiuza Barabara ya Shekilango,” alisema jamaa huyo.
Baada ya kujikusanyia data, ndipo alipowatafuta ‘vijana’ wetu ambao aliwaomba walifuate gari lake kwa nyuma kwani alikuwa akimsaka mkewe.
Haikuwa kazi rahisi kumpata mkewe kwani zoezi lilianza saa 7:05 hadi 8:25 usiku huku akifanya ‘ruti’ za kumwaga kutoka Shekilango hadi Mwenge na Mwenge hadi Shekilango.
Alipofanikiwa kumwona mkewe na kumwita kwa jina lake la Dina, ndipo akashtuka na kuanza kutoka nduki kisha kutokomea gizani akiwa na wenzake.
“Niliambiwa nikakataa, sasa nimeshuhudia kwa macho yangu, hakuna sababu ya kupindisha maneno. Nilimlipia mahari karibu ng’ombe tisa, atakapofika nyumbani ataikuta talaka ikimsubiri,” alisema Ombeni akionekana mwenye hasira.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kuwa kwa sasa kuna ongezeko kubwa zaidi la wanawake wanaouza miili yao maarufu kwa jina la machangudoa, kisingizio kikubwa kikiwa ni ugumu wa maisha.

Saturday, December 22, 2012

DAWA YA PENDAPENDA

MTANZANIA JOYCELYNE AIBUKA KIDEDEA MISS EAST AFRICA


Joyceline akiwapungia mkono mashabiki baada ya kutangazwa mshindi.
Joycelne (wa pili kushoto) akipongezwa na mshiriki mwanzake.

Washiriki wakipita jukwaani katika vazi la ufukweni.…

Joyceline akiwapungia mkono mashabiki baada ya kutangazwa mshindi.
Joycelne (wa pili kushoto) akipongezwa na mshiriki mwanzake.
Washiriki wakipita jukwaani katika vazi la ufukweni.
Warembo wakiwa mbele ya kamera.
Mambo yote ni kujinadi.
Kivazi cha ufukweni kikitamba.
Majaji wa shindano hilo wakifuatilia mpambano.
Kundi la The Voice likitumbuiza.
  Mrembo ‘akiuza’ sura.
Mrembo akionyesha alivyojaliwa na Subhana.
Walioingia Tano Bora.
Jocelyne akijielezea kabla ya kutangazwa  mshindi.
  Mad Ice akiserebuka na shabiki wake.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi (katikati).
Gari aliloshinda Jocelyne.
MSHIRIKI wa Tanzania katika Shindano la Miss East Africa 2012, Jocelyne Diana Maro, jana ameibuka kidedea katika fainali zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

Ushindi huo umemfanya Jocelyne azawadiwe Dola 30,000 ambazo ni pamoja na gari aina ya Mazda lenye thamani ya Dola 15,000 na mkataba wa kufanya kazi na Miss East Africa Organization wenye thamani ya Dola 15,000.



SHILOLE AMKUFURU MUNGU

MSANII wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu, Risasi Jumamosi lina data kamili.

Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.

MCHANA

Majira ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha akapata…
Stori:Gladness Malya na Hamida Hassan
MSANII wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu, Risasi Jumamosi lina data kamili.
Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.
MCHANA
Majira ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha akapata nao msosi na kuwapa msaada wa vyakula.
Wakati wa mchana, Shilole alionekana akiwa ndani ya mavazi nadhifu yaliyomsitiri vilivyo binti wa Kiislamu, akila pamoja na watoto hao na wageni wengine waalikwa wakiwemo wasanii wenzake.
 
USIKU
Kweli usiku ni wa mashetani kwani baada ya matukio ya mchana, sherehe ilihamia katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo kulikuwa na matukio kibao ya kumkufuru Mungu.
SHEREHE YAANZA
Sherehe hiyo ilianza majira ya saa 4:00 usiku kwa wageni waalikwa kuanza kupombeka kwa ‘mipombe’ mikali kwani hakukuwa na zile za kawaida huku wakipata muziki mtamu wa kushushia ulabu tumboni.
JUU YA MEZA
Kufuatia kukolea kwa kinywaji, Shilole alipanda juu ya meza na kuanza kukata mauno kihasarahasara.
MASHINDANO YA KUKATIKA
Baadhi ya waalikwa ambao nao walikuwa wamekolea masanga tilalila, walianza kushindana kukata mauno huku mshehereshaji wa shughuli hiyo, Halima Haroun ‘Kimwana Manywele’ akimnyanyua mtu mmojammoja kwenye kiti na kwenda kukata mauno mbele na ambaye alishindwa, basi alitakiwa atoe Sh. elfu 50.
Katika kukata mauno, kuna baadhi ya waalikwa waliopitiliza na kujikuta wakimwaga ‘lazi’ na kucheza kwa staili ya kubinuka wakiwemo kuku watamu (mashoga) na mastaa wa filamu kama Jacqueline Wolper, Halima Yahaya ‘Davina’, Batuli ‘Neshi’, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’, Baby Candy na wengine kibao.
Pamoja na kufuru hizo pia kulikuwa na matukio mbalimbali kama ugomvi baada ya Shilole kupoteza simu na kuanza kumshushia kipigo mdogo wake anayejulikana kwa jina moja la Mary.
Pia mwanadada anayewatengeneza wasanii nywele anayejulikana kwa jina moja la Bonita, alidai kumfumania mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la Papaa akiwa chobingo na ‘mchuchu’ mwingine hivyo pakachimbika.
Hata hivyo, waliokuwa wakimwaga ‘lazi’ ni walewale waliokuwa kwenye kisomo mchana na kuonekana kusahau mambo ya dua.

MSICHANA WA MIAKA 6 AMWAGIWA MAJI YA MOTO SEHEMU ZAKE ZA SIRI

Mama mmoja mwenye umri wa miaka 26   ameusikitisha umma wa watu pale alipommwagia maji ya moto mtoto wake wa kike........

Mwanamama huyo bado anashikiliwa na POLISI kwaajili ya maelezo zaidi na wanaharakati wa kutetea haki za watoto wameonekana kulivalia njuga swala hili kwa kutangaza kumfungulia kesi mwanamama huyo

Friday, December 21, 2012

AIBU VIDEO YA MWANAUME ALIYENASWA AKIFANYA MAPENZI NA NG'OMBE

Kijana mmoja  ambaye jina lake halikuweza kufahamika  mara  moja  amenaswa  akifanya  mapenzi na  ng'ombe  zizini.....

Tukio  hilo  la  aibu,  lilitendeka  mchana  na  kushuhudiwa  na  watu  kadhaa ambao mbali  na  kumrekodakifanya uchafu  huo, walimpa kichapo  cha  mbwa mwitu  ili  liwe fundisho  kwa  watu  wenye  roho chafu  kama huyu........

Mtandao huu  unawaasa  vijana  waachane  na tabia kama  hizi maana  ni  hatari kwa afya  zao......

Historia  inaonesha kuwa   Ugonjwa   wa Ukimwi  ulimpata binadamu wa kwanza  baada  ya kufanya mapenzi na nyani....

Inasiktisha sana kuona  kuwa  binadamu wa  karne  hii bado tunafanya  makosa yale  yale ya zamani

SHILOLE ANASWA GIZANI NA MWIMBAJI WA KOFFI



MSANII wa sinema na muziki wa Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Desemba 16, mwaka huu alinaswa gizani akiwa amejiweka kimahaba kwa mmoja wa waimbaji wa mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Antoine Christophe Agbepa Mumba ‘Koffi Olomide’, Ijumaa lilimbamba.
Shilole akiwa na msanii wa Koffi.
Tukio hilo lilitokea ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, ambapo Shilole alienda kwa ajili ya kushuhudia shoo ya mwanamuziki huyo.
Akiwa ndani ya viwanja hivyo, Shilole alijikuta akishobokewa na mmoja wa wanamuziki wa Koffi ambaye jina lake halikupatikana mara moja ambapo kuna muda wawili hao walikutwa nyuma ya jukwaa jamaa ‘akiimbisha’.
Haikuweza kufahamika mara moja kama Shilole alimkubalia mshikaji huyo lakini wadakuzi wanadai baada ya shoo kumalizika, mwanamuziki huyo alimfuta tena Shilole na kuongozana naye hadi kwenye gari alilokwenda nalo pale ukumbini.


PICHA ZA USHINDI WA LEMA NA MAANDAMANO KUELEKEA MAKAO MAKUU YA CHAMA

 Lema,Mbowe na nassari mahakamani
 Mawakili wakiwa kwenye viti vyao
 Hawa ndiyo waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya lema
 Mahakamani,lissu,nassari,mwenyekiti mbowe na kilewo wakiteta na mke wa lema
 Lema akianza kutoa hotuba fupi baada ya kutoka mahakamani.kulia ni joshua nassari
 Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza
 Tundu lisu,mtetezi wa lema.aliingia baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa.ameshangiliwa sana

 Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA
 hapa lema akiwa na kilewo wakati wa maandamano ya kutoka mahakamani kuelekea makao makuu ya chadema
Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.
Imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa waliofungua shitaka dhidi ya lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.
Kwa hiyo mengine yote yamekuwa null and void.
Hukumu haikuchukua hata nusu saa.Lema ni mbunge halali wa arusha mjini tangia leo