Friday, September 20, 2013

WEZI WA MTANDAO WAKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI‏

Huyu ndiye mhusika mkuu aliyechonga mchongo wote na kumshawishi mwanamke kutumia kitambulisho chake kufanyiwa wizi huo wa kimtandao.Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani.
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi  na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi.
Mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na  kutaka kuja kurudisha line ambayo siyo yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika maelezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu Sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambayo iliwaleta mpaka ofisi za Tigo zilizopo Rozana, Buguruni.
Watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa matapeli hayo ya kimtandao.Kitambulisho alichotaka kutumia mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi ndipo mfanyakazi mmoja wa Tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi  mara moja.Aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha miioni moja kwa njia ya Sim Banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa ali-renew na kuiba pesa zake.
Hapa mtuhumiwa mmoja akiwa kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi.Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe.Wakiwa ndani ya gari la polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni.Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa Tigo, Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa mtandao.
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa



Love to hear what you think!