Wednesday, September 25, 2013

APANDIKIZWA PUA MPYA USONI


Xiaolian, 22, akiwa na pua mpya ‘iliyopandwa’ na madaktari katika paji lake la uso.
Mmoja wa madaktari walioendesha tiba hiyo akifanya tathmini ya kitaalam kwa Xiaolian.
RAIA mmoja wa nchini China anayejulikana kwa jina moja la Xiaolian, mwenye umri wa miaka 22, ametengenezewa pua nyingine na madaktari ambayo sasa imewekwa kwenye paji lake la uso, baada ya ile ya asili kuharibika katika ajali ya gari iliyomkumba Agosti, 2012. Madaktari wameitengeneza pua hiyo kwa kutumia sehemu mbalimbali za mwili wa mtu huyo zikiwemo sehemu za mbavu na ngozi yake. Operesheni hiyo imefanyika katika hospitali moja huko Fuzhou, katika Jimbo la Fujian. Wataalam hao wanatarajia kuihamisha pua hiyo na kuiweka sehemu ambapo pua yake ya zamani ilipokuwa.




Love to hear what you think!