MDADA wa Kenya anayetajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Jackson Makini ‘Prezzo’, Huddah Monroe ‘The Boss Lady’ amechanwa kuwa anatumia nguvu kubwa kujipatia umaarufu kwa kupiga picha chafu kisha kuzisambaza mtandaoni.
Mtandao mmoja wa nchini humo umeeleza kuwa, kuna watu wengi akiwemo Huddah ambao badala ya kufanya mambo yenye faida kwa jamii na hatimaye kuwa maarufu, wao hutumia njia batili ikiwemo hiyo ya kupiga picha za utupu.
Huddah katika pozi nyinine tata.
“Miaka ya nyuma ili mtu ajulikane zaidi kwenye jamii lazima afanye
kazi nzuri lakini kipindi hiki ni tofauti. Wengi hasa wadada wanajipatia
umaarufu kwa kuposti picha zao wakiwa watupu kwenye mitandao ya
kijamii. Mfano Huddah na wengine kama vile Kim Kardashian wa Marekani,”
uliandika mtandao huo.