Gari aina ya scania yenye nambali za usajiri T578 ALS likiwa na tela nambli T125 AGM lililobomoa nyumba na kusababisha vifo vya watu 3 wa familia moja |
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi hii ni miili ya watu walifariki kwa gugongwa na roli hilo |
Wananchi wa kijiji cha Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakiwa msibani |
WATU
watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa
baada Gari aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana Usiku.
Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa Tatu na Robo usiku katika Kijiji cha Ilongo Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha magari
kugongana na kugonga nyumba na kusababisha vifo na majeruhi.
Alisema
chanzo cha ajali kilitokana na Gari lenye namba za usajili T578 ALS
likiwa na tela lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania
likiendeshwa na dereva ambaye hakuweza kutambulika liligonga kwa nyuma
gari lenye namba T959 ASC aina ya Scania.
Alisema
gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Juhudi Saimon(34)Mnyiha mkazi
wa Dar Es Salaam kisha gari hilo kugonga nyumba mali ya Matia Mwagala
mkazi wa Kijiji cha Ilongo.
Aliwataja
matrehemu kuwa ni Asia Yahaya (52)mkulima na Msangu, Abubakari
Yahaya(8) Msangu na mwanafunzi darasa la pili aliyekuwa anasoma katika
Shule ya msingi Ilongo na Fatuma Yahaya (6) Msangu mwanafunzi wa darasa
la kwanza Shule ya Msingi Ilongo wote wakazi wa kijiji hicho.
Aidha
aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na Abuu Fadhil
(22)Mzigua mkazi wa Dar Es Salaam ambaye ni tingo wa gari lililogonga
Nyumba pamoja na Steven Chiwa (26) mbembe raia na mkazi wa Nchi jirani
ya Zambia ambaye ni msindikizaji wa gari hilo ambao wamelazwa katika
Hospitali ya Misheni ya Chimala.
Hata
hivyo wa dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara
baada ya tukio ambapo Kaimu Kamanda anatoa rai kwa yeyote mwenye
taarifa juu ya mahalialipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo
azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake,
vinginevyo ajisalimishe mara moja.
Wakati
huo huo Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Asajile Mwamtina
(46) mkazi wa kijiji cha Syukula Wilaya ya Rungwe mkoani hapa
akituhumiwa kufanya mapenzi na binti yake wa miaka 13.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuongeza kuwa lilitokea juzi majira ya saa Kumi na Mbili jioni baada ya
kumvizia binti huyo (jina limehifadhiwa) ambaye aliacha shule akiwa
darasa la tano mwaka 2011 kwa matatizo ya ugonjwa wa kifafa akiwa
anapika.
Alisema
mtuhumiwa alipata mwanya wa kufanya unyama huo kutokana na mkewe
ambaye mama mzazi wa mhanga huyo Tumikigwe Samalinga akiwa kijiji
cha Kiwira kuuguza mgonjwa na kuongeza kuwa taratibu za kumfikisha
mahakamani zinafanyika.
Aidha
katika tukio lingine eneo la Makunguru Jijini Mbeya Vyumba 12 vya
biasharaa viliteketea kwa moto jana majira ya saa Tano asubuhi
vilivyokuwa vimetoka kujengwa mali ya Dominick Mbinga Mkazi wa Dar Es
Salaam.
Hata
hivyo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza baada ya moto huo
kudhibitiwa kwa ushirikiano baina ya kikosi cha zima moto na uokoaji na
wananchi.
Thamani
halisi ya uhalibifu bado kujulikana pamoja na chanzo ingawa kwa mujibu
wa majirani walisema inawezekana ikawa ni hitilafu ya umeme kutokana na
muda huo wapangaji wa nyumba hiyo kutokuwepo wakati moto ukitokea ambao
ulijulikana baada ya majirani kuona.