Baada ya kuona kusitisha bunge kurushwa live kumepigwa vita, sasa wabunge wamekuja kwa staili ya matusi ili wananchi wasiwe na hamu kabisa ya kuliangalia bunge....
LEO kwa mara nyingine tena, Mh.Peter
Serukamba amesikika waziwazi kabisa akitoa tusi mbele ya bunge na hakuna
hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake.
Bila woga wala aibu ya kuwa huenda anasikilizwa na wakwe zake ,Serukamba amesikika akisema "Come-on F.U.C.K Y.O.U."

TUKIO LENYEWE LILIKUWA HIVI:
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliitaka serikali iwachukulie hatua kali wahusika wote wanaohusika na matukio ya utekwaji na uteswaji wa baadhi ya watu,kwa kutolea mifano ya Dr.Ulimboka na Kibanda.katika hotuba hiyo,kambi imeonesha kutoridhika na mwendendo wa utendaji wa idara ya usalama wa taifa.

Aidha hotuba hiyo kuna mahali imemtaja
Rwakatare na mwenendo wake kabla ya kukamatwa.
Shida imeanza pale ambapo Mh.Serukamaba aliomba mwongozo wa spika,na kusema kuwa,kuna baadhi ya maswala yaliyomo ktk hotuba hiyo( hasa kuanzia ukurasa wa 1-4) yanazungumzia kesi ya Rwakatare ambayo tayari ipo mahakamani.

Na kwamba kuendelea kusomwa kwa hotuba hiyo ingekuwa ni
kuingilia mwenendo wa kesi na kwamba hapo ingekuwa ni kuingilia uhuru wa
mahakama.
Katika kutetea hoja zao,wabunge watatu wa kambi ya upinzani(H.Mdee,J.Mnyika na T.Lisu) walisimama na kujaribu kuonesha uhalali wa hoja zao.Wote watatu walijieleza kwa kadiri walivyoona inafaa.

Baada ya hapo ndipo aliposimama Mh.Serukamba na kusisitiza
uhalali wa hoja yake.
Sasa kile kitendo cha yeye kusimama tena,inaonekana
kulikuwa na minong'ono upande wa pili(lakini hiyo haikusikika) ndipo kwa
kujisahau alipojikuta ametupia hewani TUSI HILO la "Come-on F.U.C.K Y.O.U."!
Kwa jinsi alivyotukana,aliunganisha haraka na maelezo yake kiasi kwamba Mh.J.Ndugai(aliyekuwa akiongoza) hakumkatisha, akamwacha aendelee.

Baada ya maelezo ya Mh.Serukamba,naibu spika(mwenyekiti)
alitoa kauli yake rasmi.
Ndugai amesema kuwa mgogoro huu una mtazamo wa
kikanuni,kwa hiyo ameagiza kamati ya kanuni ya bunge ikutane mara moja
kujadili swala hilo kisha itoe ushauri kwa kiti cha spika jinsi gani ya
kshughulikia mambo hayo yanayoonekana yana utata.