NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema
atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya
sekondari. Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na
baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.
Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa
Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0)
jijini Mbeya.
“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui
natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia
darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata
hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.
“Kama kweli
ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu?
Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini
nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.
Kwa miezi
kadhaa sasa Mulugo amekuwa akidaiwa kughushi vyeti na kutumia jina la
mtu ili kufikia kiwango cha elimu alichonacho madai ambayo alisema
yanamchafulia jina katika jamii.
Kuhusu suala la matokeo mabaya
ya kidato cha nne mwaka jana, Mulugo alisema matokeo hayo mabaya
yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa
wanafunzi.
Naye Ruth Mnkeni kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa
Mlugo amezindua tovuti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari
ijulikanayo kama Shule Direct.
Muluigo alisema kuzinduliwa kwa
tovuti hiyo kutawafanya wanafunzi kupata maarifa mengi ya vitabu
mbalimbali na kuinua kiwango cha elimu nchini