IMANI
za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange na Kata ya Isange
baada ya matukio ya kupotea na kuawa kwa Watoto kutokea mara kwa mara
ambapo Marehemu hukutwa wakiwa na mapungufu ya viungo ikiwemo Kichwa.
Katika
tukio la hivi karibuni Mtoto mmoja aliyejulikana kwa Jina la Lista
Sebule (8) Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mpombo
iliyo katika Kata ya Isange Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe
Mkoani hapa alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa
baada ya Siku 9 akiwa amekufa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mama mzazi wa Marehemu
Christina Sakalile alisema binti yake alipotea majira ya saa tisa jioni
Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani ili kuchaji
lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni hali iliyozua wasiwasi na
kuanza kumtafuta bila mafanikio.
Alisema
baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kijijini ambapo Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Isange Daudi Nsyani ambaye baada ya kupewa taarifa hizo
pia aliwataarifu viongozi wa Kata akiwemo Diwani wa Kata ya Isange Elias
Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Brayson Nguro ambaye
aliitisha Mkutano wa wananchi.
Mtendaji
huyo aliwaambia wananchi hao kushirikiana ili Mtoto apatikane hali
ambayoiliitikiwa na wananchi ambao walitaka Mtoto apatikane aidha akiwa
mzima ama Mfu ambapo juhudi za kumtafuta zilianza na hatimaye kumpata
Aprili 8, Mwaka huu akiwa amekufa huku akiwa hana baadhi ya Viungo.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema Mwili wa Marehemu ulipatikana ukiwa pembezoni ya
Mto Nkalisi uliopo Kijijini hapo ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo
kama Kichwa na Miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana baada ya Mbwa kukutwa
akiwa ameshika na kuudondosha baada ya kukutana na watu hali
iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza hadi Mwili wa
Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa pembezoni.
Baada
ya kupatikana kwa mwili huo Taarifa ilipelekwa Polisi ambao walifika
katika eneo la tukio na kuupima kisha kuwakabidhi ndugu kwa ajili ya
mazishi ambapo watu wawili walikamatwa kuhusika na tukio hilo baada ya
kupigiwa kura za siri na wananchi na kukutwa na kura nyingi ambapo
wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na kura nyingi.
Kutokana
na hali hiyo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo alisema mfululizo wa vitendo
hivyo unatokana na kutokuwa na Vituo vya Polisi ambapo Halmashauri ya
Busokelo inakituo kimoja kilichopo katika Mji wa Lwangwa mahali ambapo
ni mbali sana kutokana na gharama kuwa kubwa.
Kwa
upande wake Diwani wa kata hiyo Elias Mwandele alisema wananchi waache
kutembea usiku ambapo aliongeza kuwa Vilabu vya Pombe vifungwa saa mbili
usiku huku akiwataka Wazazi kutowapeleka watoto kwenye Shughuli za
Machungo ambapo wameweka ulinzi wa Sungusungu ili kudhibiti hali hiyo.
SAMAHANI
KWA PICHA HII HATUJAIONYESHA VIZURI SABABU MWILI WA MTOTO LISTA
UMEHARIBIKA VIBAYA HIVYO TUMEONA SI VYEMA KUUONYESHA WOTE
MARA
TU BAADA YA POLISI KUUTOA MWILI PORINI NA KUUCHUNGUZA WALIWAKABIDHI
WAZAZI ILI WAENDELEE NA TARATIBU ZA MAZISHI YA MTOTO LISTA
MGUU WA MAREHEMU LISTA
MWANA
USALAMA AKIWA AMEUSHIKA MGUU WA MTOTO LISTA MARA TU BAADA YA KUUPATA
MWILI WAKE PORINI NA KUKUTA HANA BAADHI YA VIUNGO VYAKE VYA MWILI
UMATI MKUBWA ULIOHUDHURIA MAZISHI YA MTOTO LISTA
Habari picha na Mbeya yetu