Saturday, December 22, 2012

SHILOLE AMKUFURU MUNGU

MSANII wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu, Risasi Jumamosi lina data kamili.

Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.

MCHANA

Majira ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha akapata…
Stori:Gladness Malya na Hamida Hassan
MSANII wa filamu na muziki Bongo asiyeishiwa habari, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kufanya kisomo na watoto yatima mchana na usiku akaangusha pati iliyokuwa na matukio ya kumkufuru Mungu, Risasi Jumamosi lina data kamili.
Matukio hayo yaliyoshuhudiwa na wanahabari wetu yalijiri Desemba 18, mwaka huu ambapo Shilole alikuwa akisheherekea siku yake kuzaliwa bila kutaja umri.
MCHANA
Majira ya mchana wa jua kali, bidada huyo alifanya kisomo nyumbani kwake Kinondoni, Dar pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Magomeni kisha akapata nao msosi na kuwapa msaada wa vyakula.
Wakati wa mchana, Shilole alionekana akiwa ndani ya mavazi nadhifu yaliyomsitiri vilivyo binti wa Kiislamu, akila pamoja na watoto hao na wageni wengine waalikwa wakiwemo wasanii wenzake.
 
USIKU
Kweli usiku ni wa mashetani kwani baada ya matukio ya mchana, sherehe ilihamia katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo kulikuwa na matukio kibao ya kumkufuru Mungu.
SHEREHE YAANZA
Sherehe hiyo ilianza majira ya saa 4:00 usiku kwa wageni waalikwa kuanza kupombeka kwa ‘mipombe’ mikali kwani hakukuwa na zile za kawaida huku wakipata muziki mtamu wa kushushia ulabu tumboni.
JUU YA MEZA
Kufuatia kukolea kwa kinywaji, Shilole alipanda juu ya meza na kuanza kukata mauno kihasarahasara.
MASHINDANO YA KUKATIKA
Baadhi ya waalikwa ambao nao walikuwa wamekolea masanga tilalila, walianza kushindana kukata mauno huku mshehereshaji wa shughuli hiyo, Halima Haroun ‘Kimwana Manywele’ akimnyanyua mtu mmojammoja kwenye kiti na kwenda kukata mauno mbele na ambaye alishindwa, basi alitakiwa atoe Sh. elfu 50.
Katika kukata mauno, kuna baadhi ya waalikwa waliopitiliza na kujikuta wakimwaga ‘lazi’ na kucheza kwa staili ya kubinuka wakiwemo kuku watamu (mashoga) na mastaa wa filamu kama Jacqueline Wolper, Halima Yahaya ‘Davina’, Batuli ‘Neshi’, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’, Baby Candy na wengine kibao.
Pamoja na kufuru hizo pia kulikuwa na matukio mbalimbali kama ugomvi baada ya Shilole kupoteza simu na kuanza kumshushia kipigo mdogo wake anayejulikana kwa jina moja la Mary.
Pia mwanadada anayewatengeneza wasanii nywele anayejulikana kwa jina moja la Bonita, alidai kumfumania mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la Papaa akiwa chobingo na ‘mchuchu’ mwingine hivyo pakachimbika.
Hata hivyo, waliokuwa wakimwaga ‘lazi’ ni walewale waliokuwa kwenye kisomo mchana na kuonekana kusahau mambo ya dua.




Love to hear what you think!