Ni wazi kabisa, hili halitawapa faraja
waamini wa Uislamu kote duniani, na kwa jinsi ambavyo tumeona migogoro
ya kiimani ikiendelea kuigubika dunia siku za karibuni, hili la sasa
huenda likafanya migogoro hii ikawa ndio mwanzo wa vita ya tatu ya
dunia. Kama huamini, sikia habari hii
Kwa mara ya kwanza katika historia ya
dunia, muumini mmoja wa dini ya kiislamu huko nchini Ufaransa,
anajiandaa kuanzisha msikiti ambao utakuwa ni mahususi kwa ajili ya
waumini wa dini hiyo walio mashoga.
Ludovic Mohammed Zahed, amejiweka tayari
kabisa kwa ajili ya kukabiliana sio tu na changamoto atakazokumbana
nazo kwa uamuzi wake huo, bali pia kwa mabaya mengine yoyote
yatayojitokeza huku akijua kuwa mambo hayo ambayo anajiandaa kuyakabili,
lazima yatamtokea. Zahed, sio tu kwamba ni muumini wa kiislamu, bali
pia ni mchambuzi aliyebobea katika imani hiyo na anajiandaa kuanzisha
msikiti huo katika mji wa Paris, mwishoni mwa mwezi huu.
Tunahitaji kuwa na sehemu ya usalama kwa
ajili ya watu ambao wanajihisi hawako salama na huru sana pindi
wanapokuwa katika misikiti ya kawaida. Wapo wanawake hawapendi kuvalia
vitambaa hadi usoni au kukaa nyuma wawapo misikitini, wapo wanaume ambao
hawana hisia za kiume na wanajihisi wanapokuwa mbele za watu
hawajisikii uzuri, na mradi huu sasa ni kwa ajili ya kuwaletea matumaini
mapya katika kuabudu.