Askari
wa Jeshi la Polisi wakijihami na matambara pamoja na mifuko ya nailoni
ili kumdhibiti mtuhumiwa aliyejipaka kinyesi mwili mzima na kutaka
kuwakimbia askari kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam leo. Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja
alidaiwa kuwa ni mwizi wa simu lakini hakimu alimwachilia huru kutokana
na kukosekana ushahidi hata hivyo askari waliendelea kumshikilia tena
jambo ambalo lili muudhi na aliporudi mahabusu aliamua kujipaka kinyesi
mwilini.
Askari wakimdhibiti mtuhumiwa huyo kwa kutumia matambara na mashuka mazito kutokana na kuwa na kinyesi kingi.
Akipandishwa kwenye gari la polisi na kuondoka nae.
Akilazimishwa kuvaa nguo.
Akiondolewa eneo hilo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.