Wednesday, 11 July 2012 20:48 |
0digg
Ester Sumira, Geita WAGANGA wa Tiba Asilia wa Kijiji cha Katoro (Uwaka), wilayani Geita, wameamua kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (Fongong’o Saccos), kwa lengo la kukopeshana fedha kuondokana na wimbi la umaskini, baada ya Serikali kusitisha shughuli zao kwa muda mrefu. Wakizungumza kwenye kikao kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake, Charles Kabaka, waganga hao walisema kutokana na kazi zao kusimamishwa kwa muda mrefu, wameamua kuunda Saccos ili kupata fedha za kuendesha maisha. Pia, walisema hatua hiyo inalenga kubadilisha na mawazo kuhusu kazi zao pale Serikali itakapowaruhusu kuendelea. Waliomba Serikali kushirikiana nao pale wanapotoa taarifa za baadhi ya wenzao wanaopiga ramli, zinalenga kuua albino na vikongwe ili kukomesha mauaji hao. Kwa upande wake, Kabaka aliomba jamii kuachana na imani potofu za ushirikina, kwani haamini kumuua albino ni utajiri na kuongeza kuwa, vikongwe wanaouawa ni wazazi wao ambao hawana hatia yoyote. Kabaka alisema chanzo cha mauaji hao ni wale waganga matapeli, hivyo iwapo Serikali ikishirikiana kuwafichua itakomesha mauaji hao na kuwafanya kuaminika kwa jamii. Naye Jastumin Mussa, alikemea tabia ya baadhi ya waganga wanaokiuka maadili ya kazi yao suala ambalo wankwaenda kinyume na sheria za nchi na kuwaomba waganga ambao hawajajiunga kwenye vikundi, kujiunge mara moja ili kubadilisha na mawazo jinsi ya kutoa huduma sahihi. |