Saturday, July 28, 2012

UGONJWA WA EBOLA WAZUKA TENA KAMPALA UGANDA


Baada ya tetesi za majuma kadha, serikali ya Uganda na Shirika la Afya Duniani, WHO, wamethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umeibuka magharibi mwa nchi

Watu kama 13 wamekufa na wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya ya Kibaale. Chanzo cha ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.

Virusi vya Ebola havina dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni homa, kutapika, na kuhara.Ugonjwa huo ulizuka Uganda miaka 12 iliyopita, na kuuwa watu zaidi ya 200.



Love to hear what you think!