Kaimu Balozi wa Venezuela nchini Kenya ameuawa mjini Nairobi.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje nchini Kenya wamesema wanaamini kuwa alinyongwa katika makazi ya ubalozi huo. Balozi Fonsekka alikuwa ametumikia katika wadhifa huo kwa siku 12 tu.
Polisi wamethibitisha kuwa wafanyakazi wawili wanahojiwa kuhusiana na kifo cha mwanadiplomasia huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57, hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
source http://dewjiblog.com