Selemani Msindi ‘Afande Sele’.
MFALME wa Rymes, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ amefungukia ishu ya
yeye kugombea ubunge kwenye Jimbo la Morogoro mwaka 2015 na kusema kuna
wabunge wawili wanamshashiwi kuchukua uamuzi huo kutokana na mambo
wanayoyafanya.Akipiga stori na blog ya Millardayo, Afande Sele alisema kuwa ni wengi wanaomvutia katika hilo lakini hasa ni Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Halima Mdee wa Kawe na Burhani wa Lindi.
Alisema: “Mtu kama Zitto Kabwe ni mtu ambaye ananipigia simu mara nyingi na kunishauri, namheshimu sana, yuko pia dada Halima Mdee. Hawa wananionyesha kitu flani ambacho naweza kukifanya vilevile, kwa kifupi wengi wanaonivutia wapo vyama vya upinzani,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Kuna vyama saba vya kisiasa vilivyoniita nijiunge navyo kugombea Ubunge lakini viwili ndiyo vyenye nafasi kubwa ambavyo ni Chadema na CUF.