Sunday, September 30, 2012

MABINTI WAWILI WA WASSIRA WAJIUNGA CHADEMA



Esther Wassira Watoto wa kike wa waziri wa nchi ofisi ya Rais Mheshimiwa Stephen Wassira, wameamua kutokuwa wanafiki kwa kuamini chama tawala cha baba yao na kuchukua kadi za uanachama wa CHADEMA.

Mabinti hao ni pamoja na muimbaji aliyewahi kutamba na wimbo wake ‘Sheila’ Esther Wassira na dada yake Lilian Wassira.

“Imefikia wakati tunahitaji kuona mabadiliko Tanzania kwasababu haitoshi kukaa na kusikia vilio vya watanzania kila siku, ukipita kote wanasema maisha magumu, serikali haifanya chochote, migomo maandamano yamekuwa yakizidi,” alisema Esther ambaye ni mwanasheria wakati wa kupokea kadi hizo mbele ya katibu mkuu wa chama hicho Dr. Wilbrod Slaa.

“Katika sehemu kama hiyo tuliyofikia watanzania wanachohitaji ama mahali popote katika nchi kinachohitajika ni mabadiliko almost katika kila sekta. Kwahiyo mabadiliko hayo kutokea hayawezi kutokea kama tutabaki na malengo yale yale, sera zile zile, mifumo ile ile , uongozi ule ule, tunahitaji vitu vipya.”
Naye Lilian alisema, “Mienendo ya hiki chama nimeifuatlia na nina imani nao, nimesikiliza sera zao na nimezielewa.

Sifuati ukongwe wa chama na hiki chama kina mizizi ya akina nani. Nafuata chama kwasababu kwanza mwamko walionao, sera zao za movement for change na jinsi nilivyoona hawaongei tu lakini tumeona wazi.

Tunaona yaani wanavyopambana, tunaona na tunajua kwanini ilikuwa vile, sisi si wajinga. Sasa kwasababu tunaona,na sisi tumeamua tuwe sehemu ya CHADEMA.”

SHILOLE NA AUNT EZEKIEL WAFANYA BALAA KUBWA NDANI YA MAKONDE BEACH CLUB



SHOW ILIANZA KAMA MIDA YA SAAA SITA HIVI HEBU CHEKI PICHA ZA SHOW HIYO ILIVYOKUA









Thursday, September 20, 2012

AIBU : MATITI YA BABY MADAHA YAANIKWA NJE KAMA KARANGA


STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amejikuta akiumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya matiti a.k.a nido zake kuchomoza na kuonekana hadharani akiwa jukwaani na kusababisha midume yenye ukame kumzengea.

Tukio hilo la aibu isiyo na kipimo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu usiku wa kuamkia Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako kulikuwa na tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012.
Baby Madaha alifanya kioja hicho baada ya kutakiwa kupanda jukwaani kuimba na Juma Kassim ‘Nature’ ambaye wameshirikiana katika moja ya nyimbo zake.


Bila hiyana, Baby alipanda stejini kwa mbwembwe na kujikuta akimwaga radhi kwa kuonesha matiti hadharani na kusababisha umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe huku mwanadada huyo akiendeleza libeneke la shoo kali.


Baada ya kushuka jukwaani ndipo dada huyo alipovamiwa na wanaume wakware ambao walimbonyeza Kizenji hadi alipookolewa na mabaunsa na kupelekwa nyuma ya jukwaa.

Wednesday, September 19, 2012

WAZIRI MKUU WA ZIMBABWE (Tsvangirai (60) ) AOA MWANAMKE MWINGINE

   Tsvangirai na mkewe (Elizabeth) wakivishana pete ya ndoa.
   ...Wakipigana busu.
   ...Wakiwasalimia wageni waalikwa.…
  Tsvangirai na mkewe (Elizabeth) wakivishana pete ya ndoa.
  ...Wakipigana busu.
  ...Wakiwasalimia wageni waalikwa.
...Wakitembea kwa madaha.
HARARE, Zimbabwe
WAZIRI Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, Jumamosi iliyopita alioa mwanamke mwingine katika sherehe ambayo haikufanyika kiserikali.
Tsvangirai (60) ambaye  amemwoa Elizabeth Macheka (35), hakuweza kufunga ndoa kamili kiserikali kwa vile kuna mwanamke mmoja aliweka zuio la kufanyika kwa ndoa hiyo akidai waliwahi kuoana kimila.
Mke wa kwanza wa kiongozi huyo, aliyeitwa Suzan alifariki akiwa na umri wa miaka 50 katika ajali ya gari mwaka 2009.

Tuesday, September 18, 2012

WEMA AACHA MAKALIO NJEE



                                                Huyu ni Anti Ezekiel








Huyu ni Wema Sepetu

MAKALIO YA WEMA SEPETU YAKIWA NJE TENA


MSANII wa filamu bongo asiyeishiwa vituko Wema Sepetu, baada ya kutangaza kuwa anatarajia kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kucheza filamu moja na rafiki yake aliyewahi kumleta nchini Omotola, sasa hana tena dili la kushiriki filamu moja na mwanadada huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa na tabia ya kujiskia sana.

Chanzo cha kuaminika kilichozungumza na mtandao huu kwa sharti la kutotajwa jina, kilidai kuwa msanii huyo anashindwa kuwaeleza ukweli watanzania kuwa hawezi tena kukutana na msanii huyo, kwani anaona aibu kutokana mambo makubwa aliyoyafanya wakati alipomleta msanii huyo.




Kila anavyoangalia umati Wazimu unampanda.Hatimaye akaanza vituko vyake.





Hapa ndipo Wema Sepetu alipoanika makalio yake tena

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Wema alikuwa na urafiki wa karibu sana na msanii huyo lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ukaribu wao unapungua na kuna uwezekano mkubwa Omotola akawa amebandilisha namba ya simu na hata email kwani haoni mazungumzo ya mara kwa mara kama ilivyokuwa awali.

“Kuna wakati alitangaza kuwa anataka kwenda kucheza filamu moja na msanii huyo lakini hizo habari sasa zimekufa na hakuna kinachoendelea kwani hawana mawasiliano yoyote na kitu kikubwa kilichotokea ni kwamba Omotola alimsoma Wema tabia yake na alihisi ni mtu wa kujisikia sana,” akilidai chanzo hicho.

Hata hivyo chanzo hicho kiliongeza kuwa kitendo kingine kilichomkatisha tamaa msanii huyo ni kutokana na skendo mbalimbali za Wema ambazo amekuwa akisoma kwenye mitandao kitu ambacho anaona wazi ni kwamba kinaweza kusababisha filamu ikauza upande mmoja wakati yeye anafanya kazi za kimataifa.

“Omotola alipokuja siyo kwamba alimpa uhakika wa moja kwa moja kuwa atamtumia kwenye filamu yake hapana, kitu ambacho alikifanya ni kuchukua baadhi ya filamu ambazo Wema amecheza na kuondoka nazo na alidai atakapolizika atamjulisha lakini hadi sasa kimya,” aliongeza.


Bwana harusi aliyekufa ghafla azikwa, majonzi yatawala msibani amuacha Mke na Ujauzito



Baadhi ya ndugu na jamaa wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa bwanaharusi mtarajiwa marehemu Rashid Hamad, kabla yaq maziko jana. Marehemu alikufa kwa ajali ya umeme masaa machache kabla ya kufunga ndoa huko Ukonga Mazambalauni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha na Prona Mumwi)
Na Stella Aron
HATIMAYE aliyekuwa bwana harusi mtarajiwa Bw. Rashidi Omary aliyekufa ghafla saa chache kabla ya kufunga ndoa ya Kiislamu na Bi. Kuruthumu amezikwa jana.
Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Kimanzichana Mkuranga ambapo Bi. Kuruthumu alishindwa kuhudhuria mazishi baada ya kuzimia na kukimbizwa hospitali.

Umati mkubwa wa watu ulishiriki mazishi hayo wakiwemo madereva na makondakta wa daladala ambao walifahamiana na marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi ya ukondakta.

Vilio na majonzi ndio yalitawala msiba huo ambao umevuta hisia za watu wengi ambao baadhi yao walizimia kutokana na mazingira ya kifo.

Marehemu Omary alifaki ghafla juzi usiku wakati familia yake na ile ya Bi. Kuruthumu wakiwa kwenye mkesha wa ndoa iliyotarajiwa kufungwa juzi saa saba mchana.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, baba mkubwa wa marehemu Bw. Ally Hatibu, alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika kwani marehemu hakuwa akisumbuliwa na kitu chochotekabla ya kupatwa na umati. "Leo (jana) saa 10 kasoro, tumemzika katika makaburi ya familia

Kimanzichana na hakuna taarifa zozote kutoka kwa daktari na hatuna hisia za mtu kuhusika na kifo hiki,” alisema Bw. Hatibu.

Aliongeza kuwa, juzi usiku marehemu akiwa na rafiki zake, alikuwa akicheza rusha roho na baada ya muda aliamua kwenda kuoga kwani alikuwa amechaduka sana na baada ya kuingia ndani, muda mfupi alipiga kelele akisema “mama yala nakufa”.


Kutokana na mayowe hayo, walikimbia ndani na kumkuta akiwa chini na hali yake ilibadilika ghafla hivyo walimkimbiza katika Zahanati ya MICO iliyopo Mzambarani.

Madaktari walishauri akimbizwe katika Hospitali ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambako nao walishauri apelekwe Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.

“Tulipofika Amana, wauguzi walimwingiza wodini na baada ya dakika chache, tulipewa taarifa kuwa bwana harusi amefariki dunia hivyo hata chanzo cha kifo chake familia hatuelewi,” alisema.

Alisema jana familia hiyo iliuchukua mwili wa marehemu hospitali, kuupeleka nyumbani kwao Mzambarauni Shule na kwenda kuzika.
Hata hivyo, kwa mujibu wa maeolezo ya mwanafamilia mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema upo uwezekano wa marehemu kunaswa na umeme kwani eneo alilokuwa amesimama kulikuwa na soketi yenye shoti ya umeme na mwili wake ulikuwa na maji.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, Bi. Kuruthumu alikuwa na ujauzito wa marehemu. 
Majira


MAGAZETI YA LEO SEP 18


.
.
.
.
.
.
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.