Hilo liliibuka juzi mjengoni katika kipindi cha maswali na majibu ambapo
Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi Mtanda alitaka kujua hatua
zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tabia za watu maarufu
kupiga picha zisizo na maadili kisha kuziweka mtandaoni.
Katika kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia alisema: “Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo
wanachukuliwa hatua stahili ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni
kinyume na maadili.”
Katika kuonesha kutoridhika na majibu ya waziri, Mheshimiwa Mtanda
alipopewa nafasi aulize swali la nyongeza alisema: “Mheshimwa spika
nahisi swali langu halijajibiwa ipasavyo. Nilichotaka kujua ni hatua
ambazo zimechukuliwa kwa baadhi ya watu mastaa kama vile Wema na Diamond
ambao hupiga picha zao zisizofaa kisha kuziweka mtandaoni.”
Kufuatia swali hilo, Nkamia alisimama na kujibu kwamba, serikali imeweka
mikakati na njia sahihi za kukabiliana na tabia hiyo na kwamba wale
ambao watabainika watachukuliwa hatua zinazostahili.
Licha ya majibu hayo, bado wabunge walionesha kutoridhika, hali ambayo
Spika Anne Makinda aliiona na yeye akaongezea “Waheshimiwa wanataka
kujua na za hivi karibuni zilizovuja mtandaoni” ambapo jibu la Nkamia
lilikuwa:
“Mheshimiwa kuhusu hizi picha za juzi zilizosambaa mtandaoni,
tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata
mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilikotokea