POLISI mwanamke nchini Uingereza, PC Gail Crocker (46), alijiua siku
za karibuni baada ya kuandika ujumbe mfupi wa simu (meseji) kwa mpenzi
wake akimshukuru kwa “burudani” waliyofaidi walipokutana kwa siri –
lakini, kwa bahati mbaya, aliituma meseji hiyo kwa mumewe.
Katika meseji hiyo, Crocker aliandika kwamba: “Ningependa tuwe
tunafanya hivi kila mara.” Tukio la wawili hao lilitokea wakati mumewe
Crocker akiwa safarini kibiashara.
Uchunguzi uliofuatia tukio hilo la kujiua kwa Crocker ulibaini kwamba
baada ya mumewe kurejea nyumbani huko St Stephen, Cornwall, ulizuka
ugomvi na mwanamke huyo mwenye watoto wawili alikunywa vidonge vingi na
kufariki.
Na mumewe, Peter Crocker (49) alisema: “Gail alikuwa ndiyo maisha yangu.”
Chanzo: METRO