Friday, September 27, 2013

WASANII 10 WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA PESA NYINGI ZAIDI 2013 KWA MUJIBU WA BONGO 5

Biashara ya muziki Tanzania imeendelea kupanuka kwa kiasi kikubwa, na wasanii wenye hits, majina, connection, bahati na sababu zingine wameendelea kuingiza fedha nyingi kutokana na muziki wao.
04a9c8c6d7a044cf8b6da3176e0d4fe4
Njia kubwa na za uhakika zinazowapatia mapato wasanii ni pamoja na malipo ya show, malipo ya ringtones, endorsements (mfano kuwa mabalozi wa brands mbalimbali na kufanya matangazo) na wengine kupata kipato kupitia biashara walizozianzisha.
Kama njia kubwa zingine mbili za kuwaingizia kipata wasanii wengi duniani zingefanikiwa nchini, wasanii wetu wangekuwa mbali zaidi. Njia hizo ni mauzo ya albam za muziki na malipo ya mirahaba kutokana na matumizi ya nyimbo zao kwenye kumbi za starehe na kwenye vituo vya radio au TV.
Licha ya kuwepo kasoro hizo, bado Bongo Flava imebadilisha maisha ya wasanii wengi.
Bongo5 imejitahidi kukusanya kadri iwezavyo, data za uhakika kutoka kwa watu walio karibu na wasanii kadhaa wa Tanzania kutaka kufahamu, kiasi walichoingiza, malipo waliyoyapata mwaka huu na data zingine zingine, kuandaa orodha hii ya wasanii 10 walioingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.
Wafuatao ni 10 waliongiza fedha nyingi zaidi mwaka 2013.

1. Diamond Platnumz
1016243_622850427736775_2127148511_n
Hakuna ubishi kuwa, mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha nyingi zaidi. Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi. Kwa uhakika, mwaka huu pekee, Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1.
Kwa show za ndani peke yake, Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2. Hivyo tangu mwaka uanze, Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki. Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu, show ya Burundi na Congo, show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa), show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita.
Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi, ukiachana na zile za kawaida, Diamond aliingiza shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi milioni 10. Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara hiyo.
Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013, show za promotion za Tigo na makampuni mengine, Tamasha la Matumaini, show ya Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club, show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi kufurika.
Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show, Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi milioni 20. Kwa mujibu wa Push Mobile, akaunti ya Diamond kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote wa Bongo Flava.
Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi.
1239507_650218681669184_1372786191_n
Ikumbukwe pia, Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi, lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100.
584fe16a273711e3b8f522000a1fbce9_7
Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio Africa.
2. Lady Jaydee
1238789_10151593260760025_1742196233_n
Huwezi amini, vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi, bali pia limempa fedha nyingi mno. Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100. Haikuishia hapo, albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake.
Hits zake mbili, Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo, zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi zaidi pia. Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25.
Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu, Foolish Age, show yake kwenye Miss Tanzania 2013, Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili, Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia, Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja.
June mwaka huu pia, Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini, iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge, imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula, vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi.
Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.
Coke Studio Africa – the new, exciting music show featuring incredible live performances by the very best in Africa
3. AY
421451_10150581514944221_264981067_n
Humsikii sana rapper huyu kwenye show za Tanzania. Tofauti na wasanii wengine, fedha anazoingiza AY zinatokana zaidi na endorsements na biashara zake anazofanya. Pesa nyingi alizoingiza zimetokana na mkataba wa mwaka mmoja na Airtel wa ubalozi uliokamilika mwezi May mwaka huu.
Katika ubalozi huo wa Airtel Africa, AY aliungana na wasanii wengine watatu wa Afrika ambao ni pamoja na Papa Wemba, Tuface na Daddy Owen wa Kenya. Katika mkataba huo AY alilipwa dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 129.
Rapper huyo wa ‘Machoni Kama Watu’ ni balozi pia wa bia ya Peroni ya Italia na kupitia mkataba huo, AY ameingiza mkwanja mwingi. AY pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha Mkasi kinachoendeshwa na Salama Jabir. Kipindi hicho kina wadhamini wawili, Cocacola na Airtel na hivyo kupitia mgawanyo wa mapato, AY amekuwa akiingiza pia fedha ya kutosha.
AY ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment inayojihusisha na kuandaa show, matangazo, kuleta wasanii wa nje na mambo mengine. Mwaka huu pekee, ikishirikiana na kampuni ya SK Entertainment, kampuni yake imeandaa show kibao zikiwemo zile zilizofanyika Elements Lounge ambapo Avril, Prezzo, Huddah Monroe na J-Martins wamewahi kuhudhuria.
Maisha ya kawaida ya rapper huyu ndio yanayowafanya watu wengi wasijue ukubwa wa kile anachokiingiza. Macho yake ameyaelekeza zaidi kwenye uwekezaji na anawekeza haswaa. Kuna tetesi kuwa, AY anajenga ghorofa lake maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anasemekana kuwekeza pia mkoani Mtwara alikonunua ardhi ya kutosha. Mungu ndio anajua ni wapi alikowekeza tena.
4. Ommy Dimpoz
e23fe27c081911e3a88722000a1f90d0_7
Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi milioni 81.
Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo, tayari Ommy ameshaingiza shilingi milioni 50. Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas, Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama zote. Watu 1,770 walihudhuria show hiyo.
Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi, amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili Music Tour.
Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5, Ommy alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine. Hivi karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.
5. Madee
7203_294710874001268_1825630445_n
Hii inaweza kuwa surprise kwa wengi lakini Madee ni mfano tosha wa jinsi single moja inavyoweza kubadilisha maisha ya msanii. Tangu atoe single yake, Sio Mimi, Madee ameshaingiza si chini ya shilingi milioni 200.
Mwaka huu ameshafanya show 10 za kampeni ya Tigo ambapo kila moja alilipwa shilingi milioni 3, show 15 za Airtel kwa kiwango hicho hicho. Alifanya show mbili za kampeni za Coca Cola, ile ya uzinduzi wa Coke Zero na Cocacola Bonanza Mlimani City. Bado ameendelea kufanya show za Fiesta 2013. Madee pia alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Fuse ODG iliyofanyika September 7 kwenye viwanya vya ustawi wa jamii jijini Dar es Salaam.
6. Mwana FA
IMG_1010 (800x534)
Mwanzoni mwa mwaka huu, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA alikuwa msanii wa tatu miongoni mwa wasanii waliongiza fedha nyingi kupitia malipo ya miito ya simu, RBT ambapo aliingiza shilingi milioni 18. Alifanya show mbili kwenye Kili Music Tour ambapo aliingiza si chini ya shilingi milioni 7 pamoja na show kadhaa za Fiesta 2013.
Show yake ya The Finest ilimuingizia shilingi milioni 19. Hivi karibuni alichukuliwa na kampuni ya Vodacom kuzunguka baadhi ya mikoa kwenye kampeni yao na CCBRT kuhusiana na kukuza uelewa wa tatizo la Fistula na kulipwa mkwanja kama balozi wa kampeni hiyo.
Mwaka huu FA amefanya matangazo kadhaa ya Vodacom. Hivi karibuni pia aliingia kile kilichoonekana mkataba kama balozi wa simu za Samsung Galaxy Tanzania japo haijulikani kama ulikuwa mkataba wa ubalozi kama ilivyo mingine.
Mwana FA pia amefanya show za nje zikiwemo za Kenya na Afrika Kusini aliyofanya siku ya Eid mwezi uliopita. Kama wasanii wengine pia, FA ameingiza fedha nyingi kwa show za kawaida za hapa nyumbani na zile za promotion.
7. Chege
3ec62770206d11e382b622000ae912ed_7
Mwaka huu Chege peke yake alifanya show sita nje ya nchi ambazo kila show alilipwa shilingi milioni 4. Akiwa na Temba ambao kwa pamoja hutoza shilingi milioni 6, Chege amefanya show zaidi ya 30 zikiwemo zile za Fiesta, za promotion mbalimbali na zile za kawaida.
Mwezi ujao yeye na Temba wataanza tour ya miezi mitatu barani Ulaya ambapo show ya kwanza itakuwa nchini Sweden, October 5. Pamoja na hivyo, Chege ana biashara ya salon.
8. Profesa Jay
1010701_10151711560347558_1761716231_n
Profesa Jay aliingiza shilingi milioni 20 za Kili Music Tour, alifanya show kubwa ya Jose Chameleone April mwaka huu, show kibao za promotion za makampuni, show ya kampuni ya IPP kwaajili ya Walemavu, Diamond Jubilee mwezi January, na show zingine za kawaida za Dar na mikoani. Pia nguli huyo wa rap ya Tanzania ameingiza fedha nyingi kupitia show nyingi za Lady Jaydee.
Prof J amewekeza kwenye biashara ya salon ambayo tayari inafanya vizuri na ameshafungua studio ya kurekodi muziki iliyopo kwenye hatua za mwisho kuanza kazi. Jize aliingiza pia fedha kupitia kampeni ya magazeti ya Mwananchi kwa kufanya matangazo na show za mikoani.
9. Nay wa Mitego
53c24b9c156c11e3959e22000aeb1b4e_7
Tangu mwaka uanze, Nay wa Mitego ameshafanya show zaidi 20 zilizomuingizia si chini ya shilingi milioni 60. Show hizo ni pamoja na zile za promotion za makampuni ya simu, show mbili za Muziki Gani, show ya Kili Music Tour, show za Fiesta na zile za kawaida. Pia ana biashara zake ambazo kwa pamoja humuingizia si chini ya shilingi milioni 4 kwa mwezi.
10. Temba
2648cdb8274f11e3a2f822000a1f985f_7
Fedha nyingi alizoingiza Temba mwaka huu zimetokana na show walizofanya pamoja na Chege. Ukitoa muziki, Temba pia ni mfanyabiashara na anamiliki duka la vifaa vya ujenzi.
Source:Bongo5.com



Love to hear what you think!