Kwenye Exclusive interview na
millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia
tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na
ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana
waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za
kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja
cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria
na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria
anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya
abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na
kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna
wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka
kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo
nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua
wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja
kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo
mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue
nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue
nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama
watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo
kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa
walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka
sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection
walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika
kulivuruga sana begi lake.
Unataka kupata stori kamili? sikiliza
AMPLIFAYA ya Clouds FM leo saa moja usiku, pia kwa Breaking News, habari
yoyote ambayo ni habari, vituko, vichekesho, videos na music na
mengine… jiunge kuwa mwanachama wa millardayo.com kupitia facebook
https://www.facebook.com/millardayo au twitter
https://twitter.com/millardayo pia instagram.com/millardayo ili uwe wa
kwanza kutupiwa link kila tukio linapoandikwa.