Saturday, May 4, 2013

Wabunge wa CCM wanapojibu Hoja za Wabunge wa Upinzani kwa niaba ya Serikali!

Imekua sasa ni Jambo la kawaida kabisa kwa Wabunge wa CCM kujibu hoja za Wabunge wa Upinzani hususan CHADEMA, badala ya Serikali kujibu.

Tulishuhudia juzi katika Hotuba ya Wizara ya Mali Asili na Utalii iliyowasilishwa na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo Mch Peter Msigwa. Katika hotuba hiyo iliyokua ikielezea jinsi Katibu Mkuu wa CCM Abdrahaman Kinana anavyohusishwa na Ujangili wa Tembo hakuna hata Mbunge mmoja wa CCM aliechangia kwa kuomba au Kuiyagiza Serikali Kuchunguza yale yaliyosemwa na Mch Peter Msigwa kama yana Ukweli ili Serikali imchukulie hatua Katibu huyo wa CCM!

Wemgi wa wabunge hawa wa CCM waliishia Kurusha Vijembe kwa Msigwa na Kumtetea Kinana na Serikali. Tulimuona Emmanuel Nchimbi waziri wa mambo ya ndani akiwa wa kwanza kumtetea Kinana, badala yeye akiwa kama Waziri mwenye Dhamana na Mambo ya ndani ya Nchi kumuomba Mh Peter Msigwa huo Ushahidi dhidi ya Kinana kuhusika na Ujangili wa Tembo. Alifikia hata hatua ya Kumkashifu Msigwa na sio yeye tu hata Wabunge wengine wa CCM walichofanya ni Kujibu hoja za serikali na Kumtetea Kinana.

Kazi ya Bunge ni kuishauri kuiamuru na Kuisimamia Serikali katika mambo yote yanayohusu maswala ya Nchi na Wananchi kwa ujumla. Ila kwa Bunge la sasa imekua tofauti kwani wanachofanya Wabunge haswa wa CCM ni KUITETEA serikali na kuchukua nafasi ya Serikali Kujibu Hoja za Wabunge hususan wa CHADEMA.!

Ndio maana Serikali imekua haiwajibiki kwa Wananchi ipasavyo kutokana na kundi hili la wabunge wa CCM kuisaidia kujibu hoja za Wapinzani. Kuna haja katika Katiba ijayo Waziri asiwe Mbunge ili hili tatizo la Wabunge wa chama kinachounda Serikali wasiwe wanawatetea Mawaziri kwa kua tu wanatokana na chama chao..!


Love to hear what you think!