Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda
mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com, kutoa maelezo kuhusiana na
barua ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) aliyoiweka kwenye
mtandao wake.
Fifa ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia na baadaye
kutoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua
ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga ambaye hakutaka barua
hiyo ichapishwa katika vyombo vya habari hapa nchini.
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa
katika mkutano wa waandishi wa habari dhidi ya Rais na TFF uliofanyika
hivi karibuni jijini Dar es Salaam mara baada ya shirikisho hilo kupokea
barua ya Fifa, ambao
Dauda alihudhuria, Tenga alibainisha kuwa barua
hiyo hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa bila ya
kuondoka nayo.
“Hata hivyo wakati Rais Tenga anazungumza na
waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya Fifa
ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pekee.
“Jambo la kushangaza baada ya siku chache barua hiyo
ilionekana imewekwa katika tovuti ya inayomilikiwa na Shafii Dauda,” alisema Wambura.
ilionekana imewekwa katika tovuti ya inayomilikiwa na Shafii Dauda,” alisema Wambura.
Alisema kufatia hali hiyo TFF imemtaka Dauda kutoa
maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba na
akishindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Dauda alisema akiwa kama mwandishi wa habari
anajukumu la kuandika habari za uchunguzi hivyo baada ya TFF kukataa
barua hiyo isichapishwe katika vyombo vya habari ilibidi afanye
uchunguzi ili kujua kilichoandikwa ndani yake.
“TFF baada ya kupata barua hiyo walituita kutueleza walichoagizwa na Fifa huku wakikataa barua hiyo
isichapishwe katika vyombo vya habari na mimi ndipo nilipoamua kufanya uchunguzi wangu ili kujua kuna nini
kingine kilichoandikwa ndani ya barua hiyo ambacho TFF hawataki kijulikane,” alisema Dauda.
kingine kilichoandikwa ndani ya barua hiyo ambacho TFF hawataki kijulikane,” alisema Dauda.
Alisema pamoja na TFF kumutaka atoe maelezo ya
mahali alipoita barua hiyo ndani ya siku saba hato weza kutaja
alipoipata kama maadili ya taaluma yake ya Uwandishi wa habari yanavyomtaka pindi anapo andika habari za uchunguzi
na hadi anakufa. (Iwapo uongozi huo wa Yanga itatoa kiasi hicho cha
fedha basi kila mchezaji atakuwa amevuna shilingi5 milioni.
source; mwananchi
source; mwananchi