Hivi karibuni Chris Brown amekuwa akimzungumzia sana Drake kwenye interview anazofanya na sasa Drake amefunguka kwa upande wake.
Miaka
kadhaa iliyopita wakati Chris & Rihanna walikuwa wameachana, Rih
alidaiwa kuanzisha uhusiano na Drake na hawajawahi kukanusha.
Kwakuwa Drake na Chris walikuwa washkaji, kitu hicho kiliwafanya wawe
na beef kiasi cha mwaka jana kupigana kwenye club ya usiku. Rapper huyo
wa “Started From the Bottom” jana alifanya mahojiano na Elliot Wilson
na kuzungumzia issue yake na Chris.
Kwenye interview hiyo Drake alimuita Chris kuwa ni mtu asiyejiamini
kwakuwa (Drake) muziki wake ni bora zaidi na kwakuwa Rihanna aliingia
kwenye anga zake.
“Kwa chombo chochote cha habari huko nje, msiniulize lolote kuhusu
huyo jamaa nikija huko. Mwacheni. Msitekwe na kutojiamini kwake.
Kutokujiamini kwake ni sababu natengeneza muziki mzuri kumzidi, nafanya
vizuri kuliko yeye.
Katika wakati mmoja wa maisha mwanamke anayempenda
alijileta kwangu na nikafanya kile mwanaume wa kweli angefanya na
kumtreat kwa heshima.