PADRE WA KANISA KATOLIKI AUAWA KIKATILI KWA KUPIGWA RISASI ZANZIBAR
Habari
zilizotufikia hivi punde ni kwamba Padre Evarist Mushi wa Kanisa
Katoliki Zanzibar ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi tatu kichwani leo
asubuhi. Padre Evarist alikuwa anakwenda kuongoza ibada takatifu katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Teresia lililopo Mtoni Zanzibar. Marehemu
alikuwa anakaribia kanisani majira ya saa 1.30 asubuhi na ameuawa mbele
ya waumini wa kanisa lake. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali
pema peponi. AMEN