Wanafunzi
hao wakielekea kwenye kituo cha polisi huku wakiamriwa kunyoosha mikono
juu baada ya kuwekewa mtego na kunaswa pamoja na kupigwa mabomu
kutokana na kulazimisha kufanyika kwa mkutano wao na kamanda Kova mbele
ya kituo hicho cha Polisi
Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda. |
|
|
Utakwenda Tu! |
BAADA
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa
maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo
ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa
na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya
utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova
aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya
tarehe 30 mwezi huu.