MSANII wa filamu bongo ambaye pia ni mtangazaji Christine John ‘Sintah’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa hawezi kuanika mali zake hadharani na watu wakazijua.
Wapo baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakitangaza mali zao, ikiwemo
ulimiki wa nyumba, magari au makampuni, ambapo kwa mwanadada huyo
imekuwa tofauti kwa madai kuwa bado hajafikia hatua ya kuziweka mali
zake hadharani.
Alisema kuwa hawezi kusema ana mali nyingi au anamiliki vitu vingi
vinavyomuigiziapesa bali vipaji vyake ndiyo utajili wake kwani mbali na
filamu pia ni MC, mfanyabiashara, Balozi, pia ni mtangazaji lakini ishu
nyingine anazofanya alidai ni siri yake.
“We suala la kuanika mali bongo hukawii kuambiwa fisadi na kama huna
kabisa utaambiwa umefulia sitaki mie, lakini kwa wanaojua maisha yangu
wanajua ila kwa mashabiki wangu kweli napenda kuwambia maisha yangu ni
ya kawaida” aliongeza.