MSANII wa sinema na muziki wa Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Desemba 16, mwaka huu alinaswa gizani akiwa amejiweka kimahaba kwa mmoja wa waimbaji wa mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Antoine Christophe Agbepa Mumba ‘Koffi Olomide’, Ijumaa lilimbamba.
Tukio hilo lilitokea ndani ya Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, ambapo Shilole alienda kwa ajili ya kushuhudia shoo ya mwanamuziki huyo.
Akiwa ndani ya viwanja hivyo, Shilole alijikuta akishobokewa na mmoja wa wanamuziki wa Koffi ambaye jina lake halikupatikana mara moja ambapo kuna muda wawili hao walikutwa nyuma ya jukwaa jamaa ‘akiimbisha’.