Muimbaji Abubakar Katwila aka Q Chief amekiri kuwa alikuwa mtumiaji
wa madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka miwili na hivyo kumharibia
maisha yake.
Hata hivyo amesema amefanikiwa kuacha kutumia miezi saba iliyopita baada ya kutumia muda mwingi kufanya ibada.
Akiongea kwa uchungu katika mahojiano exclusive na kipindi cha XXL
cha Clouds FM, Chilla amesema hakuweza kusema wazi jambo hilo kwakuwa
aliogopa kuwaumiza watu zaidi.
“Nilifikiria kwanza kabla ya kuconfess kwamba hata nikiconfess I know
there are a lot of people who care about Q Chief na wasingependa
kumuona yuko hapa katika hali hii lakini pengine ukawaamiza zaidi,”
alisema.
“Nimepitia mambo mengi katika maisha yangu lakini I don’t want to blame anyone, I wanna be responsible for my own failure.”
Japo alikataa kusema, Q alisema kitu kingine kikubwa zaidi ya madawa ya kulevya kilichompelekea yeye kufika hapo alipokuwa.
Kupitia mahojiano hayo Q Chief ametambulisha wimbo wake mpya uitwao Butterfly.