Tuesday, November 20, 2012

KALA JEREMIAH ATOA NAFASI KWA MASHABIKI WAKE KATIKA REMIX YA WIMBO WAKE WA "DEAR GOD"



Rapper Kala Jeremiah ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake Dear God ametoa nafasi moja kwa mashabiki wake kufanya remix ya wimbo wake huo baada ya kukunwa na uwezo wao wa kucomment kwa vina kila siku anapoweka status ukurasa wake wa Facebook.


Katika maelezo yake ambayo ametutumia, Kala anasema mashabiki wake wamekuwa wakimtumia mistari ambayo hata yeye mwenyewe ameshangazwa na uwezo wao mkubwa sana.

“SIKU HIZI KILA SIKU NIKIPOST KITU CHOCHOTE KWENYE PAGE YANGU YA FB, MASHABIKI WANGU WANACOMENT KWA VINA. TENA KWA VINA VINGINE KAMA AMBAVYO MIMI NIMEMALIZIA KWENYE WIMBO WA DEAR GOD. CHA KUFURAHISHA ZAIDI WANATOA MISTARI AMBAYO HATA MIMI MWENYEWE NASTAAJABU YANI MISTARI MIKALI MPAKA NATAMANI NINGEIPATA MIMI WAKATI NAUTUNGA ULE WIMBO’’

Baada ya kugundua kuwa wana vipaji ameamua kufanya remix ya ngoma yake hiyo lakini anasema itakuwa remix tofauti sana na haijawahi kutokea duniani kote.

“Tunaitaji wanawake 10 na wanaume 10 kuchana kwenye hii remix na utaratibu utakao tumika kuwapata hao watu 20 utakuwa kama ufuatavyo Jumatano hii tutaweka namba za simu kwenye page yangu ya facebook watu ambao watataka kushiriki watapiga na kujitambulisha majina yao namba za simu na kisha kuchana mistari yake atayotaka iingie kwenye remix hii na wakati anachana tutakuwa tunarecord moja kwa moja baada ya hapo tutaipitia mmoja baada ya mwingine ili kuchukua aliyefanya vizuri,” yanasema maelezo yake.

“Wale waliofanya vizuri tutawapigia simu kwa namba ambazo watakuwa wamezitaja,ambao tutakuwa tumewachagua watapewa utaratibu wa kwenda kurecord ndani ya studio za Smart Music zilizopo Tabata Barakuda.

 Ikumbukwe kila mtu atatakiwa kuchana mistari minne tu na ikumbukwe pia huu wimbo hauta pigwa hewani ila utakuwepo kwenye album yangu inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi ujao.”


Love to hear what you think!