PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu
za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na
jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa uarabuni.
Wolper amesema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze
kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka tena kuwa na mpenzi wa Kibongo.
“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani
moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda
kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na
aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas