Kijana aliyenusurika katika tukio hilo, Jacob William akilonga na Mtandao huu jinsi wenzake wawili walivyopoteza maisha.
Kijana aliyenusurika katika tukio hilo, Jacob William akilonga na Mtandao huu jinsi wenzake wawili walivyopoteza maisha.
Dada
na mama mzazi wa marehemu Mwalimu Mohamed ‘Monga’ wakilia kwa uchungu
wakati wakihojiwa na mwandishi wa Mtandao huu (hayupo pichani).
Baba mzazi wa marehemu Issa Bakari, Bakari Issa (kulia) akiwa nyumbani kwa marehemu Mwalimu Mohamed ‘Monga’.
ILIKUWA ni vigumu kuamini kwa familia ya mzee Bakari Issa na ile ya
Arafa Mohammed, wakazi wa Kigamboni, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam
baada ya kupata taarifa kuwa vijana wao wamefariki dunia wakiwa kazini,
Mikadi Beach Camp wakati wanazibua chemba ambayo ilikuwa imeziba kwa
muda mrefu.Mtandao huu ulitinga eneo la tukio ili kujua ukweli na chanzo chetu cha habari kilisema marehemu hao waliagizwa na viongozi wao wa kazi kuzibua chemba kwa ujira wa shilingi 150,000.
“Vijana walioteuliwa kufanya kazi hiyo ni Issa Bakari, Mwalimu Mohamed ‘Monga’ na Jacob William lakini inasemekana chemba ilikuwa na urefu wa futi nane kwenda chini.
“Walioingia shimoni na kufariki dunia ni Isaa Bakari (24) na Mwalimu Mohamed ‘Monga’ (29) ambapo walianza kufanya kazi hiyo saa nne usiku huku wakiwa wanatumia balbu ya umeme,” kilisema chanzo.
Aliyenusurika katika tukio hilo ni Jacob William ambaye alipozungumza na Mtandao huu alisema aliokolewa na Issa Bakari wakati huo Mwalimu ambaye ni marehemu akiwa ndani ya shimo kabla ya kufariki kwa kukosa hewa.
Alisema Bakari baada ya kumuokoa yeye aliingia tena shimoni ili kumuokoa Mwalimu lakini hakurudi, hivyo kufariki wote wawili.
Alibainisha kuwa marehemu hao walikuwa ni
marafiki wa karibu, ambapo Issa alikuwa na moyo wa peke ndiyo maana
alijitoa kutaka kuwaokoa ila kwa bahati mbaya naye akaangamia.