Ijumaa ya August 17 2012 na
ijumaa nyingine kabla ya hii ya August 17 zimekua siku mbaya kwa Madame
Rita Paulsen Big boss wa Benchmark Production ambayo ndio muandaji wa
mashindano ya Bongo star search.
August 17 shoti ya umeme
imemsababishia hasara sio chini ya milioni hamsini za kitanzania baada
ya nyumba iliyokua inatumika kama stoo ya vifaa vya production Benchmark
kuteketea yote kwa moto pamoja na vitu vilivyokuwemo ndani.
Madame amesema shoti ya umeme
ilitokana na transfoma ambayo ipo karibu na ofisi yao Kawe Dar es salaam
ambapo ofisi yote ilikua iungue ila shoti ilipofika kwenye ofisi kubwa
umeme ulijizima wenyewe kutokana na vifaa kifaa maalum kinachoweza
kuzuia shoti, hivyo nyumba ndogo ya stoo iliyokua na vifaa vya
productions vilivyokua vinatumika kwa miaka kumi Benchmark production
ndio ikateketea.
Tanesco wamethibitisha kweli
kwamba ajali ya moto imetokana na shoti ya umeme ambapo zimamoto
walichelewa kufika kwenye eneo la tukio kwa zaidi ya saa moja na nusu
huku wakisema foleni barabarani ndio iliyosababisha, hakukua na njia ya
kuuzima huo moto hivyo Madame Rita na timu yake walibaki wakitazama tu
nyumba ikiteketea.
Nilipomuuliza Madame kuhusu msg
niliyotumiwa ya uwezekano wa BSS kusimamishwa kutokana na hiyo ajali ya
moto, namkariri akisema “nahisi huyo jamaa labda alikua anataka hivyo
lakini BSS haiwezi kusimama kuruka hata siku moja, hata nikifariki”
Amesema anategemea wenye nyumba hiyo watakua wana insurance.
Kuhusu tukio la ijumaa
iliyopita kabla ya hii ya August 17, Madame Rita amesema “wezi
waliniibia begi langu lenye vitu vingi vya thamani, shilingi milioni
tatu pamoja na kadi za benki, vitambulisho na funguo za gari Mercedes
Benz ambayo mpaka sasa haliwezi kuwaka kwa sababu ufunguo ndio nilikua
nao huo huo wa spea hivyo ilibidi libebwe mpaka nyumbani, walinipokonya
wakati nimesimama nazungumza na mtu”
Madame alisha ripoti polisi
lakini mpaka sasa hajapata chochote kati ya vilivyoibiwa, ameomba yeyote
anaehusika arudishe tu hizo funguo hata kwenye ofisi za Clouds Fm
mikocheni, aweke kwenye bahasha na hata akiandika Millard Ayo zitamfikia
kwa sababu anashindwa kulitumia gari sasa hivi na inambidi aagize
funguo mwingine kwenye kampuni ya Benz Ujerumani kitu ambacho kitatumia
muda mrefu.
source; millardayo.com