MISS WORLD 2012/2013 NI MCHINA Yu Wenxia
Mshindi wa shindano la urembo la Miss
World ni Yu Wenxia kutoka nchini China. Ushindi huo umetangazwa muda
sio mrefu jijini Ordos nchini Mongolia ambapo mshindi wa pili ametokea
Sophie Elizabeth Moulds wa kutokea Wales na mshindi wa tatu akiwa
Jessica Michelle Kahawaty wa Australia.
Yu Wenxia mwenye miaka 23, ni mwanafunzi wa muziki ambaye anadhamiria kufundisha muziki pia.
Washindi kutoka Africa waliopeta katika mashindao hayo ni warembo kutoka
Kenya na South Sudan, ambapo Kenya alifanikiwa kutinga mpaka Nusu
fainali za shindano huko mrembo kutoka South Sudan akifanikiwa kufikia
hatua ya finali.
Tangu hatua za awali, mrembo wa South Sudan alionekana kushiriki na
kufanikiwa katika michuano ya Beach Beauty, pamoja na shindano la Top
Model.
source ujanatzblogspot