MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Tabora, leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya
kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu
(CCM) kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka jana.
Shauri
hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na msimamizi wa uchaguzi huo, Protace
Mgayane.
Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. |
Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 mwaka huu chini ya Jaji Mary Nsimbo Shangali.
Akizungumza
na Tanzania Daima kwa njia ya simu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya,
Silvester Kainda, alisema kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilipanga
hukumu hiyo isomwe Agosti 20 mwaka huu, lakini kutokana na tarehe hiyo
kuangukia Sikukuu ya Idd, hukumu hiyo itasomwa leo.
Wakili
wa mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, alizungumza na Tanzania Daima
kwa njia ya simu jana na kusema kuwa zaidi ya malalamiko 13
waliyawasilisha katika mahakama hiyo.